April 26, 2009

Mjumbe hauawi jamani, nami nimeyakuta

nimeikuta hii picha katika kompyuta hapa ninapoandika hili jambo, kwahiyo ili kushirikiana na wenzangu naona ni vema nami nikaiwasilisha kwenu wadau. suala lenyewe ni RICHMOND ile kampuni iliyosababisha kutetereka kwa serikali yetu. sina mengi ila jionee mwenyewe, nani yuko katikati nani yupo kulia na mengineyo. imetengenezwa na jamaa wa Mzumbe chuo kikuu kama alivyoandika hapo juu. kazi kwenu

6 comments:

  1. sina hakika kama kweli jina la mtengenezaji la picha hii ni kutoka katika chuo kikuu cha mzumbe kwani bado naamini watumiaji wa majina bandia ni wengi. kilichonivutia ni sanaa ya utengenezaji huo ambayo kwa uhakika ninaisoma sana siku hizi.
    sasahili la kuiweka picha katika mazingira hayo kwakeli sijui na siwezi kusema ili niliwasilisha kwa makusudi ya kujadili nayi waungwa

    ReplyDelete
  2. Kaka Mpangala ahsante kwa picha hii!hii wenyewe wanaiita artistic reflection of reality. Sina nia ya kuichambua sana picha hii, lakini kilichofanyika hapa ni kujaribu kusymbolize kilichomtokea Yesu wa Nazareth (kusulubiwa) na kilichowatokea baadhi ya viongozi wetu waliolazimika kujiuzuru. Sasa kinachofuata ni kujiuliza, Yesu alikuwa na maisha gani, na wale jamaa wawili mmoja upande wake wa kuume na mwingine wa kushoto, nao walikuwa na maisha gani? Then tunakuja sasa kwa wale viongozi wetu ambao wamenakilishwa vichwa vyao katika viwiliwili vya miili hii pale Golgotha, nao walikuwa na maisha kama ya Yesu na jamaa waliosulubiwa pamoja naye? Naachia hapo...

    ReplyDelete
  3. hii picha inanichekesha sana, ingawa hawa jamaa hawakusulubiwa mpaka mwisho maana waliyoyafanya yanatuumiza mpaka leo sisi wadanganyika wa nyumbani.

    ReplyDelete
  4. Anonymous10 May, 2009

    Yeah Picha inawakilisha ujumbe mzuri wa kisiasa na hali halisi ya yale yaliyotokea, lakini kwa mtazamo wangu kama mkristo huu ni udhalilishaji wa imani yetu sorry kwa kusema hivo ila nimekwazika sana kaka Mpangala.
    Ni mimi wa kunyumba Nchimbi Jr.

    ReplyDelete

Maoni yako