April 16, 2009

Yasinta+Wanablogu= MIMI NABISHA

Nilikuwa napitia mada mbalimbali ambazo nimezikosa tokana na kutokaa sana mtandaoni. Nimevutiwa na mada ya dada Yasinta kuhusu mapenzi. mada hiyo kilichonikuna ni maoni ya Prof. Mbele. kwamba tunatakiwa kutafakari kwa kina namna ambavyo tunaiga kila kitu. Kama ambavyo ameandika makala yake katika gazeti la KWANZA Jamii

Amejaribu kuhoji maendeleo ni nini na kwanini tunakubali kuitwa nchi zinazoendelea. Kimsingi kama ambavyo NABISHA kwamba magaidi pekee hawakulipua WTC mwaka 2001 bali kuna mambo yanaendelea.

Sasa katika maoni hayo nakubali kwamba yeye kama mimi nimekulia kijijini na nawaza kwa msingi wa kijijini, mtakumbuka niliwahi kundika kwamba ndege wangu amepotea. Hoja kuu ni yale yale ya kuonyeshana mbele za watu kwamba mnapendana, inawezekana kweli lakini sioni mantiki wala ulazima kama kuiga kila jambo toka kwa wazungu.

Nitaishi hivyo hata kama wapenzi wataona wamekutana mhafidhina kama rafiki zangu wanavyoniita daima. Kikubwa ni kwamba sisi kama binadamu lazaima tuwe na njia halisi za kuishi kama sisi. Lazima tukubaliane kwamba UTAMBUZI ni soma muhimu sana. ndiyo maana tunajiuliza sisi ni nani??????????? Ikiwa kama ambavyo dada Koero alivyosema kwamba siku hizi tunaiga kila kitu, nakubaliana naye akumbuke kwamba HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUFANYA NGONO KIZUNGU au hakuna anayeweza kucheka kizungu bali utacheka kama wewe ulivyo siyo wao walivyo. Tabia hii ya kuiga kwamba ni lazima kama mwenzako anahuzuni kimapenzi umfariji imeshamiri lakini haina sababu za kutokea kwake zaidi ya kuiga tu. kuna mambo yanatia KINYAA namna ambavyo tunaiga. Naamini ipo siku tutaanza KUNYA, KUTAPIKA, KULEWA, KUOGA, KUKIMBIA kizungu tena kama akina BUSH, BLAIR nk.

Lakini msingi huo wa kuiga unatokana na HULKA ambayo tunajijengea kwamba kizazi chetu chenye kuhoji ukweli kinataka hata akiwa tegemezi kwa wazazi yaani awe na miaka 17 au 20 anataka kuleta boyfriend wake au girlfriend wake nyumbani kwa wazaziwe. AJABU hivi haya ndiyo mambo tunayoyataka au ni nini? Kuiga mambo ya kijinga kama hayo au kudai kwamba kumpenda mtu kwa dhati unapaswa kuonyesha hadharani huo ni UBATILI. Kumpenda mtu kwa dhati wala hakuambatani na KULAMBANA mitaani au kujidekeza eti uhudumiwe na mpenzio kwakuwa aonyeshe anakujali. Hivi unadhani kukujali kwa kuzoa matapishi ni lazima iwe mapenzini?? Usimfanye mtu kuwa kila kitu kwako maana siku akiondoka hutakiwa na kitu!!!

Nina mengi ya kuwajuza walimwengu, naweza kuongeza hata ujinga halafu nikashindwa kujieleza vema. HEKO mzee MBELE kwa kuonyesha uhalisia, ndiyo maana nahoji hata mantiki ya ndoa zilizopo hapa duniani kwa kisiingizo kwamba kilichofungwa na mungu binadamu asitenganishe halafu anayesema maneno hayo ni binadamu mwenzio ha ha ha ha ha ha ha ha nicheke mieeeeee.
Nini kudekadeka bwana, nini ulindwe na mwanaume bwana, jilinde mwenyewe, nini kufunguliwa mlango na mwanaume???? kwani wewe umekuwa kiwete??? nini kushikwa kiunoni bwana mbele za watu, kwani huko vyumbani hakutoshi????? kwani nini washkaji??? ha ha ha ha ha a ha ha ha nawaza tu
Msikilizeni sana EMINEM hasa pale asemapo katika wimbo wake wa JUST LOSE IT halafu niambieni yule jamaa kwanini alikuwa akiishi na vitoto ndani.

ha ha ha ha ha ha leo nimeamua kuwaza zaidi. haya mawazo tu wala msikasilike washikaji maana wakati mwingine NAFYATUKA na KUBWATA. ha ha ha ha ha ha ha ha ha ooooooooooiiiiiiiiiiioooooooooo ngoja nikavue mjanhahali ndo msimu wake huu bwana.
karibuni nyasa

1 comment:

  1. Nasikitika sana kusema hivi haya mambo ya kuiga yanaenea sana siku hizi mila na desturi zetu nzuri za kiafrika zinapotea. Watu wanaangalia mno TV, na kusikiliza miziki ambayo si ya haki. Rudi nyuma kkidogo wakati ule kulikuwa hakuna TV, utamaduni wetu ulikuwa mzuri sana watu walikuwa na adabu zaidi. Siku hizi watu wanasikiliza sana miziki ambayo ni ya mapenzi na wanasoma sana mambo ya mapenzi. Na sasa ukifika huko mjini ni makelele tu hakuna kabisa amani. Yaani dunia imebadilika. Yaani sisi watu"waafrika " kwa nini tunafikiri wenzetu wazungu kila kitu wafanyacho ni kizuri? Mi bado sijajua nami vivyohivyo nimekulia kijijini jamani. Naomba mnisaidia.

    ReplyDelete

Maoni yako