April 16, 2009

HATIMAYE: Wamefika nyasa, wamefika Mbamba bay

Wamisionari,watawa au tuseme watu wa dini au vipi? lakini kumbuka usiwe na kicheko kile cha nyege za kutaka kujua kulikoni lakini tulia tu nikuhabarishe mambo ya nyasa. Chipole kuna sekondari inaitwa St Agnes ni shule ya watawa wale nadhani ni pamoja na wale wa Wabendictino wa Peramiho( dada Yasinta, sahihisha).

Wamekwisha kutua Mbamba bay na hii ndiyo hoteli yao ambayo inatwa MBAMBA BAY HOTEL. Nakumbuka yupo dada Anna pale tuliyecheza naye enzi za Mwalimu, enzi za wewe baba na mimi mama au vipi? lakini siku hizi najua amesahau hakumbuki shauri kavaa utawa jamani duuh!1 sasa habari yenyewe ndiyo hiyo kwamba wameanzisha hii hoteli au shirika la utawa ambalo ni shemu ya Chipole.
haya wageni na wwale wasiojua kuogelea na wanaogopa kama dada Yasinta(eti anaogopa mamba) Karibuni sana. tovuti yao http://www.chipolestagnes.org/ (kama sijakosea0.picha kwa hisani yao

1 comment:

  1. Kwangu sio ngeni hiyo hotel nililala hapo mwaka juzi. Ila ghalama yake ni siri yangu. Mahitaji na huduma pia usafi ni safi kabisa. Ila ni kweli kuna mamba ukifika hapa uwe mwangalifu utarudi bila mkono au mguu:-)

    ReplyDelete

Maoni yako