December 09, 2008

heee!!! warina asali nao !!!!!

TAMU ni yenye ladha ya sukari ambayo huridhisha kinywani. Ingawa vipo vitu vitamu vya kuhisia ambavyo havihitaji vipitie KINYWANI. Vitu VITAMU vipo vingi sana duniani. Havina hesabu. Vipo vinavyokolea UTAMU wake kwa kupikwa ama kuchemshwa au hata kukaangwa. Navyo huwa VITAMU, vipo vya kukorogwa kuchanganywa na kughushiwa ili UTAMU unoge. Kazi hiyo hufanywa na sisi binadamu wenye akili na busara. Lakini viumbe wengine wakiwemo wanyama, ndege, na wadudu husaidia kuifanya kazi hiyo adhimu wakati mwingine bila wao kujua.
VITAMU huwa VITAMU.
Lakini VITAMU viongozavyo na ambavyo huvivumilia vinaporishai katika GEGO na FIZI za kinywa ni asali. Lo masalaleee!! Huu ni UTAMU ulioje wa asali? Sijui unatoka wapi?. Sio wa kukaangwa wa kughushiwa. UTAMU wa maumbile. UTAMU huo wa asali si bure, umefanyiwa kazi kubwa. Haushuki duniani kama mvua Wapo wenyewe ambao wanatengeneza. Ni viumbe kama sisi waitwao NYUKI. Hivi huo UTAMU WA MAUMBILE Upoje??? mbona NYUKI wanatupatia UTAMU mpaka WARINA ASALI wasitake kujua mtengenezaji??

2 comments:

  1. Nasikia SHETANI ndio bingwa wa ofa za vitu vitamu.:-(

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa SHETANI nashindw kumwelewa kwa ujuzi wake wa kukusanya VITAMU, lakini hakuumba yeye nashangaa sana. UTAMU una wenyewe lakini ukipata OFA ya utamu basi umetenda DHAMBI heeeeee! yaani stering anakufa picha ndiyo inaanza eee bwana weee hii hatari tutapona na VIKUKU njiani? kaka Simon acha kabisa OFA za huyu jamaa ni tamu ndiyo maana nasema WARINA ASALI wala hawataki kujua nani kutengeneza asali hiyo wala hawataki kujau kwamba UTAMU kaleta nani eti DHAMBI ebooooo!
    nimeshindwa,
    dada Yasinta upo? tusaidie hapa kidogo

    ReplyDelete

Maoni yako