Mioyo yenu imo Moyoni mwangu daima
Daima nasadiki, blogu ni amani kwanu.
Nimekubali kwamba blogu imenipa mengi maishani. Nimepata marafiki wengi na daima nimwenzi mwalimu wangu Ndesanjo Macha. Nilijifunza takribani mwaka mzima kabla ya kuanzisha blogu yangu hii.
Na wakati naamua kuanzisha nawashukuru watu wote waliokuwa nami tangu zamani. Wenye kiu ya kujua namna blogu inavyotupatia wasaa wa kujifunza. Nimejifunza mengi kwa kweli. Miaka 4 nilitimiza mnamo Agosti 31 mwaka huu, ila sikupata fursa ya kuandika hapa kutokana na kukabiliwa na harakati kadhaa.
Ndipo nikaamua kutumia mikono yangu salama kutengeneza hiki. Blogu hii ilianza Agosti 2007, eneo la Sinza Kijweni,lakini wazo lilianzia kwetu nyasa ndani ya Gheto langu,mitaa ya Maliwa/Mission, eneo wanaloishi wamisionari na sisi akina kajamba nani ambao wazazi wetu walikuwa watumishi wao. Ni mtaa niupendao daima umenikuza kwa mengi jamani.
Ni mtaa ambao wazo la Upadri lilimea na kustawi kabla halijawa kimeo, kisha nikalichakachua. lakini baba ananiita Paroko hadi kesho.
nikiwa nasoma maandiko ya Ndesanjo Macha kisha niliporudi mjini nikawasiliana naye. tukapeana mbinu na mengine. hakika ikawa mwalimu mzuri, hadi enzi za kusome uandishi wa raia. nakushukuru mkubwa kwa ushauri wako.
Namshuruku rafiki yangu mtani wangu au shemeji yangu Fadhy Mtanga kunitembelea ndani ya wiki niliyotimiza siku hii. Nawashukuru sana wanablogu wote. Wale walioapata kukasirishwa na maoni yangu kwao, au andiko langu hapa basi wajue kuwa AMANI IWE KWAO DAIMA.
Nilifanya hivyo kutokana na wasaa wa kujifunza. Pia napenda sana uhalisi kuliko kujivika sura nisiyokuwa nayo, kwamba shujaa pengine ni mwoga tu niliyeshindwa kupambana na woga. Namshukuru rafiki yangu kipenzi Yasinta Ngonyani kwa kuwa nami daima kisha hata kukubali wazo langu la kuanzisha blogu ya pili ambayo kwa hakika, ilinipa ongezeko la akiba ya akaunti. Amani ya iwe nawe Yasinta Ngonyani. a.k.a mama maswali magumu. Niwashukuru nyoooteeee,
Lakini naweka ................................................................
naomba ujaze jina lako manaa sina upendeleo. Na ndugu zangu wanyasa walioniandikia baruapepe zao kuifurahi na kushauri basi nawaambia. 'Siku mapigo yangu yatakapokoma basi mjue nitakufa kwa misingi na imani niliyojiwekea. Daima nitakuwa yuleyule na ukipenda niite tu Mcharuko mwema..
Nikwambie KITU? NAWAPENDA SANA TU. ila msije mjini, kisha mtasikiliza Mandoza katika bonge la kwaito la Nkhalakatha.
ha ha ha haaaaaaaa shemejiiiiiiiii...
ReplyDeleteDogo anaanza form one we unaanza kublog...dogo anakomaa na shule weeeee kwa mbinde zote hadi anaua form four...we bado unablog...miaka 4 o'clock si kitoto..
Unajua nini shemeji? Hongera sana.... Kikwetu tunasema ukangalage ulimage...
Hakika tunasonga mbele..tunabadilishana mawazo. Tunashambuliana. Tunaelimishana. Tuna....tunaaaa........(kutangaza nia imo) tunaaaaa.....tunasonga mbele.
Hongera sana shemeji mtani.
Haya mlongo...Tuselebuke aeeee, aeeee X2
ReplyDeleteMaraha maraha kamla.
Uhenga lihengu labwina sana-
Nakupa hongera wewe na pia naipa hongera blog ya Lundunyasa kwani ni kweli bila uwepo wa blog hii Maisha na Mafanikio isingekuwepo leo hapo ndio chanzo chaka. Kama Utapata muda na kupekuwa hapa kuna makala moja inaitwa LAKINI YASINTA KWANINI? HII MADA NDO ILONIFANYA NIAANZE KUBLOG. HONGERA !!
Hongera sana Mkuu!
ReplyDeleteHongera sana Lundunyasa, hatua uliyoipiga ni kubwa sana, na sisi tupo nyuma yenu, tukijikongoja, huenda tukafikia hiyo hatua, kwani nia ipo!
ReplyDeleteTunakuombea mafanikio zaidi, na ufikie kutengeneza website!
HONGERA SANA MKUU
ReplyDeleteHongera kwa blogu yako kufikisha miaka minne. Nakuombea mingine mingi ili tupate kujifunza mengine toka kwako. Hongera sana!
ReplyDeleteHONGERA SANA KAKA!
ReplyDeleteHongera sana mlongo wangu kwa kazi nzuri unayoifanya, ni faraja kubwa kupitia humu ndani kwakweli Nakutakia kila la heri na barka nyingi ili uzidi kutuletea habari na picha zaidi kutoka kunyumba.
ReplyDeleteHONGERA SANA
DAIMA MIOYO YENU IMO MOYONI MWANGU. NAWAOMBEA AMANI IWE NANYI DAIMA. naahidi kuwa nanyi hadi siku NAFUKIWA CHINI, ngazi kwa ngazi hadi sauti na NIA itafika
ReplyDeleteheri ya kuzaliwa, lini blogu hii itakufa??
ReplyDeleteHongera sana, na pia usijali maneno ya Kamala, anatoa fwakti mahali pasipo pake, itakufa tu iwapo mwanablogu naye atakufa, sasa nani anajua siku yake ya kufa? Hata ukiamua kujiua, huna uhakika kama utakufa kweli, kwani unaweaza kuwahiwa,
ReplyDeleteKaka kamala unauliza vizuri lakini katika vizuri pana maelezo mazuri yenye uzuri ambao ukweli siyo tu uzuri wa kufa. Maana kufa ni kuzuri lakini siyo vizuri kufa kuzuri.
ReplyDelete