September 02, 2010

KWANINI tunaingiwa na HISIA ZA KUTAMANI KUFA?

Binadamu tuliumbwa kwa kusudi maalumu. Na kila mmoja yupo duniani kwa kusudio maalumu. Na kila mmoja analojukumu lake hapa duniani. Lakini binadamu tunajua kuwa Mungu anatupenda sana, ingawa hajawahi kutueleza moja kwa moja. Kwa imani twaenenda kwamba Mungu yupo nasi muda wote kwa shida na raha. Na wapo wanaojiuliza wakati wa shida kwamba Mungu yuko wapi na kwanini hawasikii?

Lakini wapo wengine wanajiuliza ni kweli UPENDO wa Mungu unafanana na ule ambao wanadamu wanaweza kuutoa. Je ni kweli binadamu wanakupenda wewe  hapo ulipo? Ili ujue wanakupenda ungependa wakufanyie nini? Na kwasababu gani wakufanyie hilo unalodhani ni upendo wao kwako? Je ni kwanini unampenda Mungu usiyemuona wakati unashindwa kuamini kuwa RAFIKI yako anakupenda? Je wema wa mungu huonekanaje na wema wa RAFIKI huonekanaje?

LABDA

Ni kwani binadamu tunaingiwa na HISIA za KUTAMANI KUFA? je maisha yetu tunahitaji yawe na furaha kila wakati?Au ni kitu gani kinatufanya uwaze hilo jambo la kusema NATAMANI KUFA? wangapi wanatamani wanatamani KUFA lakini hawajafa? Ni wangapi hawatamini KUFA lakini wamekufa? NAWAZA KWANINI WANAOTAMANI KUFA HAWAFI na wale WASIOTAMANI KUFA wanakufa?

3 comments:

  1. Kwanini watu wanatamani kufa lakini hawajafa, kwasababu mungu anaua zaidi yetu, na kila mmoja kamkudiria umri wa kuishi. Kwahiyo hata uombe vipi kama siku yako haijafika ni kazi bure.
    Swali ni je kufa ni kuwa mungu hakupendi au anakupenda? Kwasababu wanasema watu, huyu mtu kafa tunampenda, lakini mungu kampenda zaidi, kwahiyo ukifa ina maana mapenzi ya mungu ni zaidi kwako kuliko wengine wanaondelea kuishi, au?

    ReplyDelete
  2. "KWANINI tunaingiwa na HISIA ZA KUTAMANI KUFA?" Kuna wakati mtu unakuwa umechoka viungo vyote na ukashindwa kuwaza na utakachokuwa unawzaza ni kwamba hivi nipo hapa duniani kwa nini? Halafu kila kukicha majukumu hayaishi na mwisho unajisahau mwenyewe. Yaani unawakumbuka wenzako ndugu, watoto, mume/mke marafiki na wao wanaona ni wajibu wako wako kufanya hilo. Na mwisho ndo inakuwa yale maswali magumu kwali napendwa na hawa binadamu au nipo hapa kwa ajili ya nani? Na kwa nini nao wasimkumbuke huyu mwanzao? Najua hatujawahi kumsikia Mungu anasema NAWAPENDENI na BINADAMU wenzako anasema anakupenda lakini pia ni vigumu kujua kama kweli anasema NAKUPENDA. Mmmmhhh naacha ...

    ReplyDelete
  3. kufa ni kuzuri na ni muhimu kama kulivyo kuwa hai, amini usiamini

    ReplyDelete

Maoni yako