November 25, 2008

Je wajua kuhusu mimi?

Najua natamani kuumbwa nyoka ningevua magamba milele nisingezeeka, kwani nina ujanja nabasti mama Pancha. Lakini...... Nakupenda ndiyo maana nilikutaka, tulitakana, tukapendana na kuelewana. Najua miezi imepita hadi leo tumedumu lakini uchungu nilionao ni kukupoteza wewe ninayekupenda. Sina wa kumlilia ila wewe naomba unielewe, nakupenda sana usidhani nafanya dhihaka. Kicheko changu kinaficha mengi nazuia simanzi,sipendi kuonewa napenda kupenda lakini sijapendwa lakini nakulilia wewe uliniependa kwa dhati hilo najua nami nasema nakupenda ndiyo maana nakubembeleza. Hivi nini kinatutenganisha? nini kinachokusibu mpenzi wangu? kosa langu ni hilo tu, hakuna jingine? nani kakudanganya mahabuba wangu, nani kakwambia maneno au akili ya kuniacha? Ni kosa hilo tu unaniacha, ni hilo tu ndilo unakasirika kiasi hicho? nimekosa mbele za mungu na kwako pia. Nakupenda kuliko unavyodhani eti sikujali. Siyo mimi niliumbwa hivyo siyo kwamba sijali ila nakujali tatizo kwangu ni kujipa malengo na kanuni. NAKUPENDA SANA MPENZI WANGU amini nakuambia njoo tuvue samaki, tulime mihogo na mengine NISAMEHE au niambie nifanye nini ili unisamehe MACHOZI YANATOKA hakuna wa kunifuta. RUDISHA MOYO WAKO ili TUANZE UPYA, MAPENZI MAPYA, MIPANGO MIPYA
Akupendye Daima: Mnyasa wa Nyasa na Mvuvi wa samaki hodari
MARKUS MPNGALA

8 comments:

 1. kaka mpangala vipi umechanganyikiwa? kama si naomba ufafanua sijakuelewa

  ReplyDelete
 2. afafanue nini au kiswahili kimekushinda? jamaa analalamika huyu sijui kuna nini na demu wake maana mademu siku hizi vimeo sana au uwongo? lakini wnaume nao vimeo kwani wamechangia hawa wanawake kuiwa vimeo yaani kama CCM-Chai Chapati Maharage. umeona hiyo kitu imekubamba? halafu acha maswali we jamaa

  ReplyDelete
 3. Lakini sasa wote unajifanya hamfahamiki. lakini siku hizi ni uhuru kila mtu anaruhusiwa kuandika kile anachopenda na anachokifikiria au anachokiwaza.

  ReplyDelete
 4. dada Yasinta nimesoma habari hii nimeelewa kiasi lakini jamaa linafichaficha lishamba sana hili. ningekuwa mimi natafuta mademu kupitia mtandao huu.
  mimi sielewi kwanini hili jamaa linaandika haya lakini nimegundua kitu. huyu si anasema huwa anaandika makala hebu soma hapo kuhusu yeye, kwahiyo atakuwa msanii maana porojo hazikosi siku hizi. kwa mara ya kwanza nimesoma maoni mengi humu lakini naona Yasinta na huyu mwandishi wapo karibu sana mnajuana. Tusaidieni kwanza mnatufundisha nini. Mshikaji sema kama kuna sholi anakupasua kichwa mwanawane angalia usinguke. maisha kimeo siku hizi

  ReplyDelete
 5. itabidi umwuuliza mwenye blog kama yupo karibu sana na Yasinta.

  ReplyDelete
 6. Nd'o maana zinaitwa blog, magazeti tando, kila mtu anao uhuru wa kuandika anachokitaka ilimradi asivunje sheria.
  Sema kaka sema usikike,
  kwani ni vipi uhuzunike?

  ReplyDelete
 7. Mkuu usijali sana ni mambo ya mapenzi na kutakana sana si unajua mambo yakikolea uanhisi umekufa kibudu na kuzikwa marehemu fulani ha ha ha ha ha ni mambo madogo tu KARIBU SANA NYASA MKUU

  ReplyDelete
 8. Mkuu, Nyasa nshakaribia kwa sana. Ndo nshatua mabegi yangu mtani.
  Mbona hujatoa feedback ya haka ka shairi ulikokuwa unamdediketia sweety heart wa moyo wako mtamu?
  Nimefurahi kaka umefika pia kwangu. Karibu tena tusome mashairi.
  Ni hayo tu.
  Alamsiki.

  ReplyDelete

Maoni yako