October 02, 2017

MSUGUANO WA NYERERE NA IDD AMIN


NA WILLIAM KAIJAGE



●Prezidaa Idi Amin Dada akiwa kwenye shughuli ya msiba (Funeral Ceremony) ya rais Jomo Kenyatta wa Kenya iliyofanyika katika viwanja vya Uhuru Park, Nairobi Aug-1978.
●Hiki ni kipindi ambacho uhamasa wa Idi Amin Dada (rais wa Uganda) na Mwalimu Nyerere (rais wa Tanzania) ulikuwa juu kabisa kuliko kipindi chochote kingine cha historia.
● Rais Jomo Kenyatta alifariki tarehe 22-Aug-1978 (Jumanne) na kuzikwa tarehe 31-Aug-1978 (Alhamis) katika viunga vya bunge la Kenya.
●Ilikuwa ni mwaka mmoja tu tokea jumuia ya Afrika Mashariki (ya nchi 3 za Tanzania, Kenya na Uganda) kusambaratika mwaka 1977.
●Tokea mwaka 1971 Idi Amin Dada alipompindua Milton Obote, Mwalimu Nyerere hakuwahi kumtambua Idi Amin kama rais wa Uganda.
●Msiba huu ulitokea (au picha hii ilipigwa) kipindi ambacho muda wowote ingeanza vita ya Kagera (kati ya Tanzania na Uganda). Kwa kikoloni wanasema the war was imminent. Kiuhalisia miezi miwili tu baadaye vita hiyo ikaanza tarehe 30-Oct-1978 (Jumatatu).
●Watu wa itifaki ya msiba walihakikisha wanawaweka Nyerere na Amin katika kona tofauti kabisa za jukwaa ili isitokee rabsha yoyote.
●Idi Amin alikaa jirani na rais wa Liberia William Richard Tolbert Jr., Rais Abdallah wa Comoro, Prince Charles of Wales na balozi wa Uingereza nchini Kenya Stanley Fingland.
●Idi Amin Dada aliwasili eneo la tukio la msiba kwa kutembea kwa mguu kutoka hotel aliyofikia huku akishangiliwa na umati wa watu.
●Mwalimu Nyerere alifariki akiwa Uingereza mwaka 1999. Idi Amin Dada alifariki akiwa Saudi Arabia mwaka 2003.
●Mwaka 2010 watoto zao Jaffar Idi Amin na Madaraka Nyerere walipanda pamoja mlima Kilimanjaro baada ya kukutanishwa kwa mara ya kwanza Butiama mwaka 2009.
●Mengine yamebaki historia.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako