NA.
HONORIUS MPANGALA
0628994409
WENGI
wanapajua kwa jina la utani mwisho wa reli. Ni kigoma mkoa wa kanda ya
Magharibi ukiwa na sifa kemkem katika kila nyanja iwe medani ya siasa,sanaa na
hata soka. Kabila la Waha ndio wenyeji wa mkoa huo lakini yako makabila
mengine. Wako wabembe na wanyema pia. Moja
ya nyimbo bora za bongo fleva 'Leka tutigite' wa Kigoma All stars ni kati alama
ambayo inatumika kuutambulisha mkoa huo.Hifadhi ya Gombe na Mahale ambayo ina
sokwe ni miongoni mwa kivutio , pia meli kongwe duniani iliyoundwa na
wajerumani mwaka 1913 katika maandalizi ya Vita ya kwanza ya dunia MV Liemba
iko Kigoma na ingali inafanya kazi hadi Leo.
Umati wa wapenda
soka mkoa wa Kigoma wakitazama mechi ya fainali ya mashindano ya kugombea
ng'ombe katika uwanja wa Lake Tanganyika.
Historia
ya Tanzania katika soka inakwenda sawa kama utautaja mkoa huo kwa kubainisha
vilabu vilivyo wahi kufanya vyema zamani. Unaweza kujiuliza kwanini wakati huu
ambapo soka linahamasa sana hawa watu hawana timu ligi kuu kwa jinsi walivyo na
vipaji lukuki. Unapoitaja
kigoma katika soka unawataja watu kama Saidi Suedi 'Scud', Makumbi Juma 'homa
ya jiji', Edibily Lunyamila, na wengine wengi. Ukitaka mchezo wa ngumi huko
ndiko alikotokea Japhet Kaseba.
Ukitaka
Siasa huko ndiko alikotoka Zitto zuberi Kabwe na David Kafulila. Ukitaka
kufahamu kuhusu muziki huko ndiko nyumbani kwa Ali kiba, Baba levo, Banana
Zoro, Peter Msechu, Sunday Mjeda, 'Linex linenga', na Nasib Abdul 'Diamond'.
Wakati
mkoa huo ukionyesha kuwa na vipaji lukuki jambo pekee linashangaza wapenzi wa
masuala ya soka kwanini hakuna timu ya ligi kuu Kigoma. Nilifika Kigoma Mwezi
sita na kuchikonoa hoja ya ukosefu wa timu ligi kuu na wadau na wapenzi
walieleza mengi. Nikiwa nayapima maelezo yao nikaishia kutulia na kuhitaji muda
tena.
Nilifika
tena Kigoma mwezi wa tisa huu, siku zangu tatu zimetosha kujua maswali yangu
niliyouliza miezi mitatu iliyopita kwa watu tofauti na sasa nimejibiwa vilevile
na watu tofauti. Msukumo
wangu wa kujua haya yamekuja kutokana hali halisi iliyopo kutofanana na zama za
Vilabu vya RTC Kigoma, Reli Kigoma katika soka la nchi hii. Nyakati zile
ziliufanya mkoa huo kuonekana kuwa na timu ngumu na zenye vipaji halisi vya
soka. Uwepo wa mashirikia yaliyojihusisha na soka ndiko kuliko itambulisha timu
za shirikia la kibiashara kama RTC Kigoma,Kagera na Shinyanga.
Kwa
kiasi kikubwa hamasa ya wadau na imani yao pamoja na kujitoa kwao kuliwafanya
viongozi wa shirika kuona wanaweza kulitumia soka kama kutengeneza alama katika
mkoa huu. Uwepo wa Afisa biashara na masoko wa mkoa mpenda soka ndiko
kulikofanya timu kama RTC Kigoma kufanya vyema.
Haikuwa
kwa RTC pakee bali kulikuwa na klabu ya Reli Kigoma iliyokuwa chini ya shirika
la Reli Tanzania.Klabu hiyo iliyonunuliwa toka kwa klabu ya Kongo fc ambayo
ilinunuliwa na kubadilishwa jina na kuwa Reli Kigoma.
Utulivu
wa nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ni kati ya mambo
yaliyosaidi kuinuka kwa soka la mkoa huo . RTC walitegemea wafanyabiashara toka
nchi hizo mbili katika masuala ya biashara ambayo yalifanya shirika kuimarika
kiuchumi na kuwa na nguvu hata uuendesha timu. Uwepo wa Bandari na Reli
ulifanya nchi jirani kutumia bandari ya Kigoma kama njia sahihi ya kupitisha
mizigo yao na hilo lilifanya timu kutengeneza kipato na kuendeshwa vyema.
Mdororo
wa kiuchumi kwa watu wa Kigoma kunatokana na hali ya nchi jirani na kufanya
watu kutofikia malengo wanayojiwekea. Waliokuwa wakizamini na kutoa pesa kwa
ajili ya vilabu kama vya Reli na RTC. Kukosekana kwa imani kwa viongozi wa soka
nako ni sababu iliyofanya wadau kujiweka pembeni na kutokuwa na imani na
viongozi wao.
Kwa
asilimia kubwa watu wa mataifa ya Kongo na Burundi huitumia Kigoma kama sehemu
ya kufanyia Biashara na kurudi kwao. Vilabu kutokana na kuwa vyenye kuhitaji
michango toka kwa wadau na wapenzi wa soka. Mmoja ya wadau ananiambia
"kigoma kuna uswahili sana ndo maana soka linatushinda miaka hii".
Hali
ya uswahili inanifanya miweze kujua mengi ambayo yanachangia kutokufanikiwa
kuwa na timu ligi za juu.Watu hupenda kuchuma matunda pasipo kushirikia katika
kujenga vilabu vyao.Maendeleo
ya soka katika eneo husika yanahitaji watu wanaojitoa kwaajili ya timu. Hali
hii imekuea tofauti na wenyeji wa Kigoma kwa sasa.Jambo linalochukuliwa ni
kutokuwa na imani na kila mtu anayejihusisha na soka kwani fikra za wengi ni
kwamba watu hujinufaisha wenyewe pasipo kuzisaidia timu.
Uhalisia
wa yanayoendelea Kigoma ndo hayo yaliyo ifanya klabu ya Mvuvumwa kuhama toka
kigoma kwenda Dar Es salaam. Msimu uliopita klabu hiyo ikiwa katika ligi daraja
la kwanza ilipata wakati mgumu kwa mechi zake za nyumbani. Uwanja wa lake
Tanganyika kwao ilikuwa kama wako ugenini. Mashabiki na wenyeji wa mkoa huo
waliizomea na kuzishangilia timu wageni ili klabu hiyo isisonge mbele.
Unaweza
kushangaa kwanini usaliti wa klabu ya Mvuvumwa ulikuwa hivi. Lakini jibu lenye
kueleweka masikioni mwa watu ni chuki zilizojengeka toka kwa viongozi wa soka
kigoma pamoja na viongozi wa taasisi za kiserikali ambao kwa pamoja walikuwa na
lengo la kuifanya Mvuvumwa iwe chini ya KRFA ikipata sapoti kubwa toka serikali
ya mkoa na idara ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Matarajio
hayo yaligonga mwamba kwasababu mmliki wa klabu alishajua kuwa wanataka
kuochukua timu na kuifanya kuwa chini ya chama soka mkoa na mwisho wa siku I we
kama kilichozikuta RTC na Reli Kigoma. Viongozi
wengi wa soka la Tanzania katika ngazi ya klabu,mikoa na hata nchi wamekuwa na
hali ya kutumia nafasi hizo kujinufaisha katika maisha yao. Hii ndiyo iliyokuwa
'target' namba moja ya watu wa kigoma kwa Mvuvumwa fc. Viongozi wakaamua
kumwona mmliki wa Mvuvumwa kama ni msaliti wa maendeleo ya soka la kigoma na
kufanya timu ichukiwe na mashabiki.
Hali
hii imefanya timu hiyo kuhamia makao yake Dar es salaam. Na kwa kauli za
wenyeji ambao ni wadau wakubwa wa soka la Kigoma wanasema hata kama Mvuvumwa
ihamie ligi ya Kenya kamwe haiwezi kupanda daraja. Kauli hizo zinafanya nione
kuna hali ya kutoitakia mema kwa kolote kwasababu ya mmiliki wa klabu kutotaka
kuikabidhi klabu kwa viongozi wa soka mkoa.
Kwa
lililomkuta Mvuvumwa halitofautiani sana na lililowakuta Jkt Kanembwa. Baada ya
kuonekana uongozi wa klabu wote ni wa wanajeshi wale raia ambao wamekuwa waibua
hoja nyakati zote wakaanza kuwataka wachanganye viongozi wa kiraia ili kuweza
kuleta hamasa ya sapoti toka kwa mashabiki ambao ni raia.
Wakiwa
na mtazamo huo kumbe jambo lililojificha ni kwamba watu wanatafuta upenyo wa
namna ya kuingia kwenye mfumo na kuwashawishi timu ishikiliwe na Viongozi wa
chama cha soka mkoa. Na malengo makubwa yanakuwa yaleyale kuzitumia klabu
kujinufaisha kimaisha.
Watu
kama Said Sued 'Scud' walifanikiwa kuingia katika mfumo wa kiungozi ndani ya
jkt kanembwa. Kilichoendelea ni klabu kuwa na mwenendo usiolizisha na watu
kutumia klabu kama kitega uchumi na sasa inapambana ligi daraja la
pili.Kilichotokea kwa Kanembwa ndicho kilichokuwa kikimpa wasiwasi mmliki wa
Mvuvumwa anayefahamika kwa jina la Dk. Yared.
Licha
ya kuwepo kwa hali ngumu kwa uchumi wa mtu moja mmoja na akaweza kuchangia
katika klabu ili kuziinua na kuleta maendeleo ya soka lakini viongozi wamekuwa
wasio aminika mbele ya mashabiki wao. Msuguano
wa nani zaidi kati ya wale wadau wa soka wa maeneo ya Mwanga na wale wa maeneo
ya Ujiji nayo ni saababu ya kutokupata mafanikio kwa vilabu vyao kwa miaka ya
sasa. Hali hiyo inatokana na kila upande kuona wako bora katika kuufahamu na
kusimamia vyema soka kitu ambacho kinaleta au kupitisha mianya ya figisu kwa
upande wa pili.
Jambo
pekee na lenye umuhimu mkubwa Kigoma wanahitaji mabadiliko makubwa ili kuondoa
dhana iliyoko kwa wapenzinna wadau zidi ya viongozi wa soka la kigoma. Japo
wako wanaoamini uchumi wao kushuka na watu kushindwa kuchangia maendeleo ya
vilabu sababu ya mambo ya Mashariki mwa Kongo na Burundi. Napeleka fikra mbali
zaidi mbona Sudani soka linachezwa vyema ilihali maeneo mengine kukifanyika
mapigano.
Uimara
wa viongozi na wenye kutaka maendekmleo ya vilabu vyao ndio jambo linalopaswa
kuwa kichwani mwa viongozi. Soka la eneo husika husimamiwa na kupandishwa na
wenyeji wa eneo hilo. Haiwezi kutokea mtu wa Singida akaenda kusimamia
maendeleo ya soka la Kigoma. Inaweza Ndanda Kuwa na timu ligi kuu lakini Kigoma
wakakosa kwasababu ya kupingana kwa fikra kati ya wadau na viongozi kuzalisha
chuki miongoni mwao.
Soka
halina njia ya mkato,linahitaji njia iliyonyooka na yenye kuekeweka uelekeo
wake. Siasa inapitumika katika soka majibu yake ni kukosekana kwa imani
miongoni mwa wapenzi na wadau wa soka.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako