Utamu wa raha ni heshima, upendo na amani. Wawili huwa kama kumbikumbi na wengine hujiona kama JOTO na PANGABOI. Ndiyo Joto hupozwa na Panagaboi. Na yule umpendaye hakuna MWISHO haijalishi kama yuko mbali,karibu,jirani. Utamu wa roho na kupenda kwa moyo heshima ni kigezo kwani hata MOYO wako hunena kwa raha. Nikupe nini mziwanda wangu, KUMBIKUMBI wangu au nifanye nini ewe PANGABOI wangu? Moyoni najua naumia lakini naamini hakuna mwisho kwani NAKUPENDA. Najua kila MAWIO na MACHWEO hakuna MWISHO wa Penzi letu. Niambie basi nifanye nini,nikupe nini je niandike ujumbe mfupi kwako kila sekunde?Basi nina JOTO nawe ndiwe PANGABOI wangu nipulizie upepo nipe ubaridi ili nipunguze HARARA, wajua naandika huku nina simanzi? wajua kama ninasambaratika? Ooooooh nipe JOTO nikupe PANGABOI. Njoo basi tuongozane kama KUMBIKUMBI na MAPENZI yetu yadumu. HAKUNA MWISHO WA PENZI.
Akupendaye mnyasa mvuvi mahiri, mkulima satadi na mtafuta FARAJA kwako. MWAAAAAAAAAAAAAAAH
mimi Markus Mpangala wa kijijini.
NB; Asante dada Yasinta kwa Picha hii. PAMOJA DAIMA!!
Hicho ni kitu gani? nyasa kunautamu wa kusosoa
ReplyDeleteSasa mnaturingishia Kumbikumbi? Ngoja niwamwagie Senene mkome kuringa. Wale ni balaa maana dah!! Ma-vitamin na maafya yote ujuayo yako mle. Unakula ile kiasi cha kutosha wala hutohitaji mavidonge ya vitamini. Hahahahahahaha. Naja
ReplyDeleteWatu eeh, watu aah!
ReplyDeleteWatu weweeee!
Mate tu mdomoni, ngoja nighani kiduchu!
Kumbikumbi ni watamu, hata na senene pia,
Kula wanaleta hamu, nani anaebishia?
Kikosa 'tajilaumu, hakika ninakwambia,
Twapenda vitu vitamu?
Ni utamu kama nini, huo 'naousifia?
Tena wampenda nani, kila siku wamwimbia?
Kama 'kikupiga chini, kwangu 'tamshitakia,
Twapenda vitu vitamu?
Huwa havina madhara, vitamu twavyosifia?
Hivyo ndivyo vitu bora, vingine kuvizidia?
Huwa twapata hasara, kama 'sipojipatia?
Twapenda vitu vitamu?
@Markus:Naona maswala ya mapenzi ni kikohozi hapa:-)
ReplyDeleteMarkus,
ReplyDeleteUnapenda kula! Naona unawasaidia wasomaji wako kushiba kwa picha. Mambo ya Nyasa haya. Misosi. Dagaa. Senene. Mwili haujengwi kwa posta eeh!
Mtanga hivi unatunga tungaje beti kadhaa haraka haraka hivyo? Nakukubali mzee. Hebu fanya mpango ukitumie hicho kipai vizuri zaidi.
kaka we acha tu! nadhani ni vile tu napenda sana ushairi ndo maana kila nikitaka kuongelea jambo naanza kuzisikia verse zikirindima kwa head.
ReplyDeleteusijali, nitajitahidi kadiri ya nilivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kuitumia vema karama hii.
nakushukuru sana kwa kukithamini.
nawashukuru pia wote wanaoyathamini mashairi yangu.
mfanyapo hivyo huwa mnanipa hamasa kubwa ya kuendelea.
mungu awabariki sana.
du leo umetuwekea mbulika, nimezipenda sana, wamnyanja veve ukutinogesa tavayaku kuni!! mwee, mbulika kunoga, unikumbwisi kutal sana kadeni tikalihamba kudapa mbulika muviduli, usiku na taa zitu, pangi na fula yitonya,mwee, lelu unipeli kumbukumbu ya kadeni sana,
ReplyDeleteFadhy, mwanamalenga
ReplyDeletehisani,nakubalia
simanzi,wanipatia
namwibia,mahabauba
asilani,an'ache
moyoni nalo sonokeko
Simon,nipe mkono
niinue,nilipo
asilani,usin'ache
penzi kikohozi
nipige moyo konde
labda nitamweleza
asilani asin'ache
Mwenga, kwanza samaki sasa ngumbi kazi kweli kweli, yaani hapa mate yananidondoka kabisa nyasa safi sana.
ReplyDeleteMwenga, kwanza samaki sasa ngumbi kazi kweli kweli, yaani hapa mate yananidondoka kabisa nyasa safi sana.
ReplyDeletehakuna matata ni mambo ya nyasa hayo
ReplyDelete