Nikitazama nyumba kama hizi zinanikumbusha wale wanaoishi katika mazingira haya. Na kwakuwa nayakumbuka mazingira yaliyonizunguka kijijini kwetu nyasa nathubutu kusema najivunia kuishi katika mazingira ya aina hii ambayo yananipa USONGO zaidi wa kuishi kadiri niwezavyo.
Maisha ya aina hii yanasema,hayagombi,hayadanganyi,hayajutii,hayaogopi,hayakatai,hayaingilii uhuru wa mtu,hayasemi zadi ya kile kilichopo. Najivunia hili, najivuni kuyajua na kuendelea kuyaona, yananipa USONGO.Ingawaje kuna tofauti kubwa kati ya WIVU na USONGO. Lakini naamini safari inaweza kuwa na kona.
Je unajua kuwa unajua namna maisha ya binadamu wenzetu wanajua kuwa unaishi katika mazingira gani? Nitazamapo na kukumbuka nyumbani kwetu, nikiyaona haya, napata USONGO. Ni hayo tu.
Mimi pia nakumbuka sana mazingira hayo na ndio maana nimeiweka hiyo picha pale ungonini. Yaani USONGO SANA.
ReplyDeleteHata mie nimekumbuka nyumbani kijijini kwa bibi Koero. jamani umenikumbusha sana kwa bibi yangu Markus
ReplyDelete