October 27, 2017

FELA ANIKULAPO KUTI: MWANAMUZIKI ALIYEASISI MTINDO WA PIJINI KATIKA MUZIKI NCHINI NIGERIA NA KUOA WANAWAKE 27.

NA KIZITO MPANGALA

TUNASIKILIZA muziki wa Nigeria mara kwa mara na pengine huenda uliwahi kujihoji aina lugha wanayotumia kuimba na hata katika mazungumzo ya kwaida ya wananchi wa Nigeria. Mtindo huo umejaa pijini kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea kuitwa NIGERIAN ENGLISH.

Fela Anikulapo Kuti alizaliwa  mjini Abeokuta nchini Nigeria mwaka 1938. Alipewa majina OLUFELA OLUSEGUN OLUDOTUM RANSOME ANIKULAPO KUTI lakini alifupisha na kuwa FELA ANIKULAPO KUTI. Mama yake alikuwa ni mwanaharakati wa haki za wanawake katika utawala wa kikoloni wakati huo, na baba yake alikuwa ni mwalimu na vilevile alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza mweusi wa chama cha walimu nchini Nigeria. Fela ni binamu ya Akimwande Oluwole Babatubde Soyinka maarufu kama Wole Soyinka.

Fela alisoma nchini Nigeria na baadae mwaka 1958 alikwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kusoma Udakitari wa Dawa lakini alipofika huko alivutiwa na masomo ya muziki hivyo akasoma masomo hayo ya muziki katika chuo cha Trinity. Fela alikuwa mjuzi wa kupiga tarumbeta na Saxophone.

Alianzisha bendi yake iliyoitwa Koola Labitos ambayo ilipiga muziki aina ya jazz.  Huko alimuoa mwanamke aliyeitwa Remilekun Taylor na wakawa na watoto watatu. Mwaka 1963 alirudi nchini Nigeria na kuendelea na bendi yake aliyoianzisha na pia utangazaji katika shirika la utangazaji redioni la Nigeria.
Mwaka 1967 alihamia nchini Ghana na kuanzisha mtindo mpya wa muziki ambao uliitwa Afrobeat. Mwaka 1979 alisafiri kwenda Marekani na alikaa kwa muda wa miezi 10 jijini Los Angels, huko alibadili jina la bendi yake na kuitwa NIGERIA 70. Baadae alitimuliwa nchini humo pamoja na waimbaji wenzake kwa kutokuwa na kibali cha kufanya kazi nchini humo.


Aliporudi Nigeria alibadili tena jina la bendi na akaiita AFRIKA 70 na akajikita na nyimbo zilizohusu masuala ya kijamii. Alianzisha studio yake aliyoiita KALAKUTA REPUBLIC. Jina Anikulapo alijipachika yeye mwenyewe likiwa na maana ya “msimamizi wa maisha na shighuli zake”, aliamua kujipachika jina hilo baada ya kuachana na jina Ransome ambalo alidai lilikuwa ni la kitumwa, hivyo alihitaji jina lake liwe na asili ya Afrika tu.

Katika bendi yake alikuwa maarufu hasa katika uamuzi wake wa kuimba kwa Pijini, ndio maana hadi sasa wasanii wengi wa Nigeria na hata mazungumzo ya kawaida ya raia wa Nigeria yana kiingereza chenye mchanganyiko na lugha zao za asili.


Mwaka 1977 alirekodi na kuachia ngoma iliyoitwa Zombie, ambayo alikuwa ikieleza jinsi wanajeshi wa Nigeria walivyokuwa wakivamia studio yake kutokana na nyimbo zake zilizodhaniwa kuwa zinaichefua serikali ya Nigeria. Fela alipigwa vibaya sana pamoja na mama yake ambaye alirushwa nje kupitia dirishani na akaumia. Waliichoma moto studio hiyo na vifaa vyake vya muziki pamoja na rekodi ambazo bado alidai hakuziimba.

Baada ya uvamizi huo uliosababisha maumivu makali mwilini mwake aliamua kutengeneza sanduku ambalo lilikuwa kama la kuwekea maiti na akaenda nalo katika kambi ya jeshi ya Dodan jijini Lagos ambako alikuwa akiishi Rais Jenerali Olusegun Abasanjo wakati huo na kuliweka getini kisha akaanza kuachia vibao viwili hapohapo getini. Vibao hivyo viliitwa SANDUKU LA MKUU WA NCHI na MWANAJESHI ASIYEJULIKANA. Aliimba kwa majuto ya stdio yake.

Fela Anikulapo Kuti akiugua baada ya kupigwa na wanajeshi
Fela aliooa wanawake 27 wengi wao wakiwa ni wanenguaji wake katika bendi yake. Lengo lake lilikuwa ni kutosambaratika kwa bendi yake na kuonyesha kuwa ana upendo wa dhati na washirika wake, hivyo akaamua kuwaoa. Mwaka mmoja baadae alipokuwa jijini Accra nchini Ghana akitumbuiza jukwaani na ibao chake cha Zombie alitangaza kuwaacha wanawake 15 na kubaki na wanawake 12. Hilo lilizua ugomvi jukwaani na serikali ya Ghana ikampiga marufuku kuingia tena nchini humo.

Alianzisha chama chake cha siasa alichokiita MOP (Movement Of the People), mwenyewe alidai anataka kuisafisha jamii ya Nigeria hasa katika ufisadi. Chama hicho kilikuwa kinafuata falsafa za Kwame Nkrumah. Na mwaka 1979 aliingia kwenye orodha ya wagombea Uraisi nchini Nigeria lakini baadae jina lake liliondolea katika orodha ya wagombea. Alikemea mapinduzi ya ovyo ya kijeshi nchini humo. Alikuunda bendi mpya iliyoitwa EGYPY 80 ambapo alikuwa akiimba na kutukuza ustaarabu wa Misri, historia yake, maarifa yake, falsafa zake, dini zake, na utaalamu wa hisabati katika Misri ya kale.

Jenerali Muhammadu Buhari alipoingia madarakani, alimsweka jela mwanamuziki huyo kwa kuwa harakati zake zilikuwa zinaichefua serikali ya Nigeria wakati huo. Pia alituhumiwa kutakatisha fedha. Pia ni kutokana na wimbo wake ulioitwa BEAST OF NO NATION uliokuwa ukimkosoa Rais Buhari kuwa ni mnyama aliye na kiwiliwili cha binadamu kadiri alivyoona utawala wake wa kijeshi. Katika wimbo huo alioimba kwa Pijini, anasema;

“No be outside Buhari dey yee,
na krase man be dat,
animal in krase man skin ii”

fela aliamni sana mtindo wa maisha wa Afrika na nyimbo zake nyingi zlikuwa zikikosoa utawala wa kibabe katika serikali za Afrika hasa utawala wa kijeshi nchini Nigeria wakati ule. Hivy0, likaa jela kwa muda wa miezi 20 ambapo alitolewa na jenerali Ibrahim Babangida. Kisha aliamua kuwataliki wanawake 12 aliobaki nao.

Haifahamiki wazi sababu kuu ya kifo chake kutokana na hali yake kuwa dhaifu ambapo laikuwa anakonda mithili ya mtu aliyeathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI ingawa wengi husema aliathirika na ugonjwa huo kwa kuwa alisumbuliwa na kansa ya ngozi inayoambatana na ugonjwa huo.

0692 555 874.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako