October 27, 2017

WAAMUZI WA SOKA KATIKA JICHO LA JAMII.

NA HONORIUS MPANGALA
 
WAAMUZI wa soka wamekuwa wakitazamwa tofauti kulingana na wao wenyewe wanavyojiweka katika jamii ya wapenda soka. Wako ambao wameifanya fani hiyo kuwa moja ya vitu ambavyo vinaweza kuwapatia nafasi ya kucheza matangazo. Pia wapo ambao jamii imewachukulia tofauti kutokana na mitazamo yao.
Jonasia Rukyaa.
Kuna mitazamo hasi kwa baadhi ya wapenda soka waonapo waamuzi wa kike wakichezesha mchezo. Mitazamo hiyo inatokana na asili ya mchezo wenyewe unavyochukuliwa kama ni wa wanaume. Licha ya wanawake kuucheza lakini bado mitazamo hiyo imekuwa ngumu kuwatoka baadhi ya wapenda soka. Ndo maana hata wale wanawake wanaocheza soka ukiwatazama utafikiri wanaume Kwa baadhi yao.

Tanzania ina Mwamuzi wa kati maarufu Jonasia Rukyaa ambaye anafanya vizuri sana. Alikuwepo katika mashindano ya Afcon ya wanawake ikiyofanyika Kameruni. Pia baada ya kushiriki katika kliniki ya waamuzi Kule Ureno mwaka huu amekuwa na mwaliko 'appointment' ya uwepo katika kombe la dunia. Na yupo katika mshindano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya miaka 17 Iliyofanyika India. 


Wako waamuzi wengi wa kati wanawake dunia kama ilivyo Kwa Bibiana Steinhaus (Ujerumani), Amy Fear(Uingereza), Sian Massey-Ellis, Lucy Oliver (Uingereza) Fernanda Colombo Uliana (Brazil). Na hata hapa kwetu Tanzania wapo wasaidizi kama Helen Mduma, Janet Balama, Grace Wamara.
Fernanda Colombo Uliana
Kwa namna fulani waamuzi wetu wanawake wameshindwa kujipambanua katika kujiweka huru na kazi kutokana na mitazamo ya jamii. Mitazamo hiyo inatokana ni kiini cha mitazamo ya kikabila iliyopo na jinsi inavyomchukulia Mwanamke mbele ya mwanaume kama sio mtu wa kutoa maamuzi Kwa mwanaume.

Sasa nataka niwaeleze waamuzi wetu wanawake Kwa wale wa kati na wale wasaidizi. Inawezekana mtu asijue namna ya kuipata fursa lakini baada ya kuipata unaweza kujiweka katika hali ya kutazamika tofauti katika kazi yako.
Nianze na kusema jambo moja toka Kwa Mwamuzi msaidizi mwanamke ambaye inasemekana ni Mwamuzi mwenye mvuto kuliko wote Brazil. Anaitwa Fernanda Colombo Uliana. Huyu baada ya kuifikia fursa ya kuwa Mwamuzi akaamua kujitengenezea mazingira ya upekee kujitambulisha kwa wapenzi wa soka. Utambulisho huo ulitokana na mwonekano wake mbele ya mashabiki na timu pia. Baada ya kuonekana tofauti akaanza kunyatiwa na makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya Michezo na kufanya matangazo.

Waamuzi wa Brazil wanavaa sare za 'penalty' zinazotengenezwa na kampuni ya vifaa vya Michezo vya Malharia Cambuci S.A. kampuni hiyo iliwahi kuivalisha pia Klabu ya Sao Paulo na Gremio za huko. Iliingia mkataba pia na golikipa wa zamani wa Fc Barcelona Victor Valdes mwaka 2010 kama mtu anayetangaza vifaa vya Penalty.

Ujio wa Fernanda Colombo Uliana Kwa wabrazil katika uamuzi wa soka ilikuwa kama kachori kwenye mhogo uliokaangwa na mafuta. Namaanisha waliupokea vizuri kwasababu ya mvuto wake awapo kwenye mstari wa uwanja. Katika kulifanyia kazi hilo Mwamuzi hiyo alikuwa akipangwa kama 'line one'.

Kama ujuavyo 'Line one' husimama karibu na moja mabechi ya timu zinazocheza. Ikawa kama ni burudani nyingine kumwona Mwamuzi hiyo katika vazi lake huku umbo lake likiwa burudani ya macho Kwa wachezaji wa akiba na hata watazamaji wengine. Si unajua macho ya wanaume yalivyo kosa ustahimilivu mbele ya maumbo muswano ya wanawake.

Baada ya kuonekana kuvutia watu kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya Michezo ya Malharia Cambuci S.A kupitia vazi lake la penalty wakamua kumfanyia maboresho vazi la Fernanda. Hiyo ilikuwa kutokana na yeye jinsi anavyo jipambanua awapo kazini. Hadi kufikia hapo kampuni ililazimila kuingia nae mkataba wa kutangaza vazi hilo Kwa waamuzi wa kike na kuonekana mtu wa kwanza kuvaa ni Fernanda.

Fernanda Colombo Uliana
Umaridadi ule wa vazi mpya lilolokuwa kaptura ambayo mbele imefunikwa na kitambaa kingine na kuonekama mithiri ya sketi fupi ulinogesha umbo la Fernanda. 

Fifa wamefikia hatua kukubali vazi la Fernanda kutumika katika mashindano yake na huenda likaanza kutumika mwakani Kwa waamuzi wa kike kwenye fainali za kombe dunia. Fernanda alikuwa maarufu Kwa vazi lile dunia kote kwasababu fursa aliyoipata ameitumia Kwa mitazamo chanya na kufikia hatua ya kujipambanua.

Kwa jamii yetu ya kiafrika hususani Kwa taifa letu la Tanzania mitazamo ndo kitu kinacho wafanya pengine wasizifikie zile fursa ambazo walizihitaji kuzifikia. 

Nilimtazama Mwamuzi msaidizi katika mechi ya Simba na Mtibwa Dada kutokana Iringa Janet Balama nikajisemea moyoni yawezekana mitazamo inaweza mfanya asijipambanue na kuwa huru zaidi ya nimwonavyo kwenye mstari wa uwanja.

Mwili wa mwanamke umekuwa usiogusika kirahisi na wanaume katika jamii zetu. Halo hiyo inafanya hata watu kuchukuria tofauti pale Mwamuzi wa kike atakapoguswa sehemu yoyote ya mwili wake itatafsiriwa vibaya. Na hata watu jinsi na ustawi wa jamii utawasikia wakija na tamko kuwa ni udhalilishaji.

Ni Mara ngapi tunaona Mwamuzi wa kike kavaa kaptura fupi na kuchezesha mchezo. Huwa haitamkwi kama vazi lake halina staha licha kuonyesha mapaja wanasubili mchezaji akimpa mkono wa ishara ya uungwana Mwamuzi Kwa kugusa popote katika mwili wake. Wachezaji wamekuwa na mazoea ya kugusana popote iwe katika kalio au bega au kifua au ubavuni. 

Tatizo huja Kwa wapenzi wa soka wenye mitazamo tofauti na uhalisia wa tukio. Uhuru wa mwili na akili ndio ambao humpa uwajibikaji ulio bora Mwamuzi wa jinsi yoyote. Hivyo hata Dada zangu hawa wanapaswa kuwa huru na kuachana na mitazamo ya mashabiki. Kwasababu inaweza kutokea makampuni ya vifaa vya Michezo wakaja na mtindo mwingine wa sare za waamuzi wa kike. Hii ilitokea Kwa vilabu vya ulaya baada ya kuona wana mashabiki wanaume na wanawake wakaamua kuunda jezi za kuziuza kwa mwonekano wa jezi ya kuvaa mwanaume na kuvaa mwanamke. 

Natamani kuona mitazamo ya wale zi wa soka ikabadilika nikaona uhalisia wa Uhuru wa mwili mahala pa kazi kwa dadangu Mwanahamis Matiku, Jonasia Rukyaa na wenzao Helen Mduma,Janet Balama,Grace Wamara, Dalila kutokana Zanzibar na Frolentina kutokana Dodoma.

Ziko kampuni za mavazi ambazo Leo hii zinafanya kazi makocha,wachezaji na hata waamuzi kulingana na aina ya vazi ambalo anaweza kulifanyia matangazo.
Uliwahi kujiuliza umuhimu wa mashindano ya Umiss au kujiuliza kwanini katika mapambano ya ngumi kila raundi Dada mrembo anapita na bango akionyesha raundi inayofuata. 

Kwanini iwe kwao na sio wanaume. Vitabu vitakatifu vimeandika mwanamke ni pambo la nyumba sasa kushindwa kwetu kuwatengenezea mazingira ya kuwafanya watu wakahamasika na uwepo mahali Fulani ambapo mwanamke atakuwa mwendesha shughuli hizo ni akili zetu za tuliopo ulimwengu wa tatu.
Mitazamo yetu ikibadilika dhidi yao hata soka lao litakuwa na mashabiki wengi kwasababubya kutumia vyema fursa.

0628994409

No comments:

Post a Comment

Maoni yako