Mwaka 1931 Wamisionari waliomba eneo la kujenga himaya yao ya kitawa kwa serikali ya kijiji cha Lundu. Baada ya pendekezo lao serikali iliwaomba wazee wawili kutoka Ukoo wa Mpangala ili kuwapa Wamisionari hao eneo la kujenga makazi ya Kitawa.
Alikuwa
Mzee Machwembeli Mpangala (Baba yake Mzee Hansgary Mpangala au Waziri) na
Lipondelu Mpangala (Babu yake Mzee Hubungu au Robert Mpangala).Mzee Machwembeli
alikuwa anamiliki eneo la kuanzia kilipo kituo cha afya kuelekea kaskazini( Kwa
wale wanao ifahamu Lundu) na Mzee Lipondelu alitoa kuanzia Hapo kituo cha afya
kuelekea Kusini iliko nyumba ya mapadre.
1959
Walijenga machine ya kupump maji toka forodha ya Chivanga hadi eneo la
misheni.Mzee alishiriki ujenzi Huo akiwa na Bruda Lambert. Ananiambia gari ya
kwanza kufika kijijini kwetu ilikuwa ni 1954.
Asubuhi
ya Leo alinipiga na salamu ya kijerumani nikabaki natoa macho tu.Uishi miaka
mingi zaidi Mzee wangu.
Honorius
Mpangala,
#Mtoto_Wa_Misheni
No comments:
Post a Comment
Maoni yako