NA HONORIUS MPANGALA,
LUNDU
TULIANZA
safari yetu na dadangu kijijini kwetu Lundu na kuelekea Halmashauri ya Wilaya
ya Nyasa Mbamba Bay. Changamoto za barabarani hazikukosa kwasababu ya mvua
zinazonyesha. Tukifika na kukamilisha yaliyotupeleka huko.
Saa
kumi jioni nilipofika kituo cha mabasi cha Mbamba Bay sikukuta gari ya kugeuza
kwenda kwetu Lundu. Ikatulazimu tupande ya kuishi njiani, gari iliyotoka Mbinga
kwenda Kihagara. Nikiwa nawaza namna ya kutoka Kihagara hadi Lundu lakini
nikapanga jambo kuwa bodaboda ziko kila eneo sikuhizi,na sikutoa nauli ya yangu
na Dada nikamwambia waambie natoa Mimi. Nikamwambia konda natoa Kihagara kuna
mtu anatusubiri,nilifanya Kwa maksudi.
Tulipofika
Mlima wa Yungu tukielekea Kihagara dereva akasema kuna dalili ya kunyesha mvua hivyo
sitawafikisha Kihagara stendi bali nitaishia Camp yaani njia ya panda ya
Kihagara na Malongo. Tulipofika Waliposema mimi nikatoa nauli pungufu ya elfu
na mia tano nikagoma kutoa yote kwasababu sikufikishwa Kihagara.
Nilipowagusa
bodaboda kutifikisha Mimi na dadangu Lundu waligoma,niliwabembeleza wakagoma. Nikamwambia
Dada tutafanya mazoezi. Ilikuwa ni saa 2:05 tukitoka Camp tukaanza kutembea
hadi Nindai kwa kupitia njia ya Malongo. Milio ya Wanyama kama Komba ndo
ilikuwa mziki wetu,wadudu pori nao kama kawaida Kwa sababu ilikuwa ni milimani
katika msitu.
Sista
aliogopa nikamwambia hakuna jinsi nimevaa Rozari ambayo niliitoa na shingoni na
kuvaa mkononi. nikaanza na kupiga vifungu pale safari ya kutembea ikaanza. Tulikutana
na watu wawili eneo moja majira ya Saa tano na Nusu wakiwa wanatoka kulewa.
Hapo Dada alinishika mkono nikaanza kucheka maana nilimwambia mbele yetu kuna
watu wanakuja. Eneo tulilokuwa jumlisha usiku ule ndo kilichoogofya.
Nikamwambia
hatuna jinsi lazima tufike nyumbani haraka iwezekanavyo kwasababu ya kile
tulichokiendea kuwa na umuhimu mkubwa na thamani kubwa. Ni kama tulipewa
dhamana na familia fikieni na kurejesha taarifa iliyotarajiwa.
Tukiwa
tumeimaliza milima tunakaribia kufika kibao cha shule ya Liwundi saa 5: 55
usiku tukakutana na Mzee aliyebeba kafia akitoka ziwani. Nipogundua nikawa
napita kwa ukaribu zaidi ili kuweza kutambua ni wa aina gani. Muda sio tatizo
ila mashaka ni eneo lenyewe.
Dada
akauliza hapa wapi nikamwambia hii Nindai punde tunaianza Yola. Tulitembea huku
Dada akiwa ana kiu ya maji nami nikamkataza kunywa maji ya mtoni kwani yalikuwa
machafu. Ilikuwa nampa matumaini kuwa utakunywa Hapo mbele. Kiujumla aliingia
disko la kimasai kwa kusafiri na Mimi. Alichoka nikamwambia haya ndiyo majukumu
uliyopewa na kilichobebwa kinahitajika na muhimu sana kwa mustakabali wa maisha
yetu na ni haki yetu sasa usisikitike juu ya kusumbuliwa na changamoto kama
hizi kwani utawasimuliwa wale wataotaka kujua ulifanikiwa vipi hili zoezi.
Tulipita
shule ya Yola, palepale nikakumbuka nilipokuwa kule milimani kuna ‘comment’ ya
kaka Atley Mpangala kuwa nikifika Yola
niulize jambo. Licha ya kuwa usiku mkali wa saa Sita nikasimama na kuhesabu Fremu
ambazo kaka huyu aliniagiza hapo nikajua zipo 12. Tukatembea kidogo tukakutana
vijana wanne wanatoka ziwani kuvua dagaa sikuwasemesha. Tulipofika mbele kidogo
nikaona nyumba wakazi wake wako nje wanashughulikia dagaa nikamwambia Dada
twende ukanywe maji sasa.
Kutoka kushoto kwenda kulia, Honorius, Emma na Thobias Daudi. |
Dada
alipokunywa maji nami nikanywa, tukaulizwa swali mbona usiku mnaenda wapi
nikajibu tunaenda Tughi alfajiri tutaenda Lundu, sasa tukishuka gari Camp na
bodaboda walikataa kufanya biashara nasi ikabidi tutembee.
Hapo
Dada akaniambia ni saa 6:48 usiku. Nikamwambia mama mwenye ile nyumba kuwa
naomba kujua mmiliki wa zile fremu pale shule akajibu Serikali ya kijiji.
Nikamwachia agizo kuna kijana anahitaji kujua gharama za pango anaitwa Atley Mpangala yuko Dar es salaam.
Akaniambia ile familia naijua kesho nikiamka nitamuuliza Mtendaji na nitapeleka
jibu kwa nduguze ili wampigie simu. Alipouliza mbona unamtaja huyo kijana
unamjua nikamjibu Mimi ni Mpangala na nawafahamu wenzangu pia.
Tukaendelea
na kufika Mkili (Tughi) saa 7:13.Nikamwambia Dada gari hii tutapanda inayoenda
mjini hivyo tupumzike. Tukaingia ndani ya gari na kusubiri kupambazuke gari
ianze safari ya Songea kupitia kwetu. Huwezi amini gari ikaanza kuondoka saa
8:40 usiku daaaaa(Kuna watu wanapata changamoto halafu kuna anayejiita mbunge
wao kudadadeki anakoroma tu mjini huko).
Tulitembea
nasi tukafika home saa 10:50 tulipofika home moja kwa moja tukapitilizia kulala
ili asubuhi tufanye kazi iliyotufanya turudi home kwa changamoto lengo kufanya
mambo kwa maagizo ya wale waliotuagiza.
Nawaonea
sana huruma Nyie wapiga kura za wabunge wa maeneo kama haya. Bila kuwapigia
kelele hakika hakuna kitakacho badilika. Hapa utagundua moja ya changamoto
iliyojitokeza ni usafiri gari moja ikienda basi wewe utasubiri. Sasa ukiwa na
uharaka wa kutatua yale yaliyombele yako utahitaji kulazimisha.
Bodaboda
nao wakawa waoga wa kutufikisha tutakako kwasababu ya Usalama mdogo kwao kwani
barabara ina changamoto sana. Tulichofanya na dadangu ni kuvaa ujasiri na
kusema tutafika salama na mungu alijua hawa wamebeba msalaba wa wenzao acha
niwalinde wafike.
Halafu
mnasema hii serikali ya hapa kazi tu. Kazi gazi zinafanyika wapi hizo kazi
mbona wengine hawazioni. Muulize mbunge anayejiita Injinia una pendekezo gani
la kiwanda kupitia kwa uwepo wa Ziwa Nyasa na kustawi Kwa mazao ambayo yanaweza
kufanya watu wakanufaika na kiwanda atao macho tu. Halafu unakaa bungeni kupiga
makofi.
Nimebahatika
kufika mikoa 20 ya Tanganyika kila sehemu kuna changamoto zake lakini watu
wanaongea wanapiga kelele ndo maana wanafanyiwa kazi ambazo wanaambiwa hapa
kazi tu. Utafikiri tumelekezwa kuanzia serikali Kuu hadi za Mitaa.
Maendeleo
ya Nyasa ni kwa mwananchi mwenyewe lakini sio kwa huduma ambazo serikali inatoa
kwa wananchi. Ndo maana sijashangaa kukuta Benki ya NMB hadi sasa kuendea
kuhudumia kwenye gari pale mjini Mbamba Bay.
Inaumiza
halafu watu wanaishia kusifiana tuu mbele ya kamera na kusema naunga juhudi za
Fulani sijui... Hivi mnayajua Maisha ya wamachi kweli? Eti Injinia Manyanya unataka kuniambia kwa
huu nusu msimu wa uongozi wako kama mbunge umefikia nawe nusu ya ahadi zako?
Tanzania
ya nyerere tutaishia kuisoma katika makaratasi , umimi utabaki kuwa
palepale....NIMESEMA. Nimechafukwa na nyongo balaa ngoja nimpigie simu wife
kwanza!
No comments:
Post a Comment
Maoni yako