NA MWANDISHI WETU
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wametoa
msaada wa shilingi milioni 400 kwa Kituo cha Afya cha Mkili kilichopo Kata ya
Ngumbo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma
bora za Afya kwa wananchi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa barua ya wizara
ya Afya kwenda kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa (kama inavyoonekana pichani), Benki
ya Dunia imekuwa ikitoa ufadhili wa huduma za uzazi wa dharura katika vituo
mbalimbali vya afya vya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kupitia mpango huu,
miundombinu inayokarabatiwa au kujengwa ni pamoja na Chumba cha Upasuaji,Wodi
ya Wazazi/chumba cha kujifungulia, Maabara ya damu na nyumba za watumishi,”
ilisema taarifa hiyo .
Mkili ni miongoni mwa vituo 100
vya afya ambavyo vimeteuliwa kupata msaada huo kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni
jitihada za kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo na wilaya ya Nyasa kwa ujumla
wanaweza kupatiwa huduma kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako