NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Botswana kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa ya kulaani matamshi ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji kutoka bara la Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara
hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari ilisema, serikali imeamua kumwita balozi
wa Marekani nchini humo ili kutoa ufafanuzi juu ya matamshi ya Trump na kueleza
nafasi ya Botswana katika kundi lililomaanishwa na rais huyo wa Marekani.
“Leo (jana) Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imemuita balozi wa Marekani hapa nchini kutoa
ufafanuzi dhidi ya matamshi ya Rais Trump kuwa nchi za Afrika na nyingine ni
kama uchafu, katika kikao cha Kamati ya Wabunge wanaoshughulikia masuala ya
uhamiaji,
“Serikali ya Botswana pia imetaka
ufafanuzi kutoka serikali ya Marekani kupitia Balozi huyo na kuthibitisha kama nchi
yetu ni miongoni mwa uchafu unaotajwa,
“Botswana inaziomba nchi
wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika
na nchi zinazoendelea kote duniani kulaani matamshi ya rais Trump,”
No comments:
Post a Comment
Maoni yako