January 17, 2018

HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA INAO WAJIBU WA KUHUDUMIA BARABARA ZAKE

NYASA inahitaji matibabu kamili (kama dawa ya Mseto) sio kutuliza maumivu (Panadol). Matengenezo haya nimeyakuta mwezi Disemba 2017. Niliwaacha watengenezaji wakiwa kijiji cha Ndumbi, lakini yanaonekana yameanzia kijiji cha Amanimakolo (nako kunajazwa vifusi na kukarabati).
UJUMBE WANGU: Halmashauri ya Nyasa inao wajibu wa kuhudumia barabara zake wakati wote si kujaza vifusi kwakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu anapotembelea au kiongozi yeyote, au shughuli yoyote ya muda inapofanyika. Barabara ni nyenzo muhimu sana ya kukuza uchumi wa eneo lolote. Kila la heri wahusika. Tutaendelea kukumbushana.




Ukarabati wa Barabara kijiji cha Ndumbi wilayani Nyasa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako