January 17, 2018

HONGI NYASA: KISIWA KILICHOWEKWA RADA YA RAIS WA MALAWI

NA ALBANO MIDELO, LIULI

MBUNGE wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni kwenye tamasha la utalii wa Nyasa alitamka wazi kwamba wilaya ya Nyasa ni Benki ya vivutio lukuki vya utalii hali ambayo inaifanya wilaya hiyo kuwa kitovu cha utalii katika ukanda wa kusini.
 
Afisa Maliasili na Utalii wa wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo anakitaja Kivutio kingine ambacho hakifahamiki lakini ni maarufu katika wilaya ya Nyasa kuwa ni kisiwa cha Hongi kama ambavyo unakiona kwa mbali kilichopo Kata ya Liuli ambacho ni kidogo lakini chenye kilele ambacho kabla ya uhuru wa Tanganyika, Nchi ya Malawi wakati huo ikiongozwa na Dk. Ngwazi Kamuzu Banda “Wamuyaya” iliweka Rada ambayo ilijulikana kwa jina la “Taa ya Banda”.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako