January 05, 2018

AMBULANCE YA HOSPITAL YA WILAYA NYASA ILIVYONUSURIKA KUANGUKA.

NA HONORIUS MPANGALA, LUNDU
AWALI niombe radhi kwa kukosa picha kwasababu nilipofika eneo la tukio simu yangu ilizima moto. Nakumbuka nilitumia simu yangu ndogo kumweleza kakangu Markus Mpangala kuwa narejea nyumbani lakini tumesimama mahali kuna gari inasaidiwa kunasuliwa toka ilikoegema. Ni mlima wa kwanza ukitoka kijiji cha Kihagara eneo la Camp, tulikuta hiyo Ambulance ikiwa imeshindwa kupanda mlima kwa uterezi na kuburuzika hadi pembezoni mwa barabara. Jambo la kuahukuru ni kwamba ilikuja kugota kwenye jiwe vinginevyo ingelala kwa ubavu katika kuta za barabara.
Barabara ya Lituhi kwenda Mbamba Bay  eneo la mtaa wa Likwambe katika Kijiji cha Lundu wilayani Nyasa.

Gari hiyo ikiwa imebeba chanjo na dawa za ARV ikizisambaza kwa hospital ya Mkili na Lituhi, ilipata tatizo hilo majira ya saa tano asubuhi. Na haikufanikiwa kutoka badala yake ikazidi 'kuslip' hadi kwenye ukuta Wa barabara. Gari yetu iligika hapo ikitokea mbamba bay majira ya saa kumi jioni tukatoa msaada Wa kuikwangua njia kwa majembe na chepa kuondoa uterezi na baadae kusukuma hiyo gari ikapanda mlima na kufanikiwa kutoka. Ikawaza zamu ya gari yetu ikafanikiwa kupita bila shida yoyote.

Tulipofika kituo cha afya cha Mkili tuliikita ile ambulance dereva wake hana hamu ya kuendelea na safari hadi Lituhi akataka kukabidhi zile Dawa na chanjo pamoja na mizigo mingine kitu ambacho walishindwa kuelewana na kondakta wetu juu ya nauli ya mzigo. Ikabidi ambulance tuiache pale na dereva akiwaza namna ya kufika Lituhi na kurudi mbamba bay na muda ilikuwa imeshafika saa kumi na mbili jioni.
Jambo ambalo lilinifikirisha ni ile Chanjo na ARV labda pengine ilihitajika haraka lakini tatizo la barabara lilofanya gari ikwame kwa muda Wa masaa 6.
Katika gari alikuwepo Diwani Wa kata ya lituhi, nilimuuliza swali halmashauri ya Nyasa mnahudumia barabara ngapi zilizo chini yenu,huwezi amini hakuweza kujibu akasema sijui. Yawezekana alifikiri kuwa jibu lake la sijui litamwondoa katika wimbi la maswali ambalo angepata. Nikazidi kumhoji hii barabara unajua iliaanzishwa mwaka gani hakujua pia akatokea mzee mmoja akajibu kuwa tangu mwaka 1961.

Palepale nikamuuliza Tena kwahiyo kesho waathirika Wa VVU wanaochukua Dawa hospital ya lituhi itabidi wabadili muda Wa dozi kwasababu Leo gari ndo hii imekwama na haifiki safari leo. Alichoniambia kuwa lile eneo ni eneo la diwani George Ndimbo ambaye ni Wa kata ya kihagara,mi nikamwambia namjua kwasababu nilimchapa sana makwenzi shule akiwa kidato cha kwanza Mimi nilikuwa cha tatu St Paul's. Akaduwa,nikamuuliza hivi nyie madiwani Wa tarafa ya luhuhu mbona mmelala kiasi hiki tatizo nini ugumu Wa kazi au uelewa Wa kufanya kazi sababu ya madarasa. Hapo aliona kama nimemtukana kwasababu niliambiwa yeye ni wa level ya darasa la saba.
Hapa lengo sio kutambuana kwa elimu lakini hii iwafikie wote waliko,katika tarafa zilizoko wilaya ya nyasa. Hakuna tarafa ina shida za kimawasiliano kwa barabara na simu kama tarafa ya Luhuhu wako wanaosema angekuwepo ' Ng'osi' labda leo hii isingekuwa hivi. Hapa alitajwa ng'osi Marehemu Komba.
Mmoja Wa abiria alidiriki kusema " Natamani wazee washushe mvua ya elfu kumi maeneo ya Buruma,Nyoni,Ndengu hadi Nangombo.Ili ule msafara ukakwame na ushindwe kunasuliwa kwa Masaa mengi" . Abiria Wa pili akasema " Aheri roli ya mzigo ikachore saba Buruma na ule msafara ushindwe kufika unapotaka kwenda,"
Wakati natafakari mauizio hayo nikajiuliza yaani haya maombi yote ya Hawa watu ni kutokana kutoridhika na kile wanachokipata kama Huduma toka kwa Wakuu. Meli ya mizigo MV njombe na Ruvuma yawezekana zikawepo mbamba bay baada ya kuanza safari zake jana katika bandari ya Itungi. Hii keki kama itagawiwa sawa basi hapa patafanana na Buseresere, Katoro, Runzewe, Bwanga, Kiangaiko,Butiama, Msoga na kwingineko.
NYEPESI NYEPESI ZA KISIASA
Aliyewahi kuwa diwani Wa kata ya kihagara Mzee Pata alikuwa chama cha Chadema. Lakini kwa kipindi ambacho kata iko chini ya Ccm mzee Pata kaamua kurejea CCM kwa mtindo uleule Wa wale Wa Arusha. Ila sasa huyu Pata ye anasema " Kama ameniita na kunipa milioni tatu na pikipiki,halafu kadi sijanunua Nina hasara gani' . Kumbuka hapo kuna mtu anamwelezea na yeye Pata ni mwenyeji wa Kihagara.
Jioni nitakuletea ya Kimahakama.
5/1/018

No comments:

Post a Comment

Maoni yako