September 05, 2007

Unakumbuka 'inshu' ya Dito au umesahau

Jamaa hapa ananidokeza ndogo ndogo za mjini Mbinga na maeneo mengine ya nchi hususani Darisalama eti kuna jamaa wandai haki katika kesi zao kama ilivyokuwa kwa mtuhumiwa wa m******** ya kijana wa daladala huko Darisalama,ndugu Dito mzuri.

Jamaa wanaona kesi yao haitendewi haki hivyo wanatumia jina la Dito angalu kudai kile wanchoita haki.Lakini hivi haki ni nini hasa?mbona watu wanalalamika sana suala hilo.
Inawezekana kuna namna ambayo kila raia anapaswa kumiliki haki hiyo hata hivyo imetoweka na kuchukuliwa na watu mithili ya dito,mimi sijui maana kazi yangu kuvua samaki kwetu nyasa lakini suala la sheria namwachia Ndesanjo anajua hizo kesi ni nini.

Hta kama atabeza kazi kwake maana ye' ni mwanasheria mahiri tu.kama humjui hebu zama hapa www.jikomboe.com

3 comments:

  1. sijui lakini naamini kila kitu sasa kinakwenda kama walivyopanga kwani hakuna lolote linaloendelea hapa

    ReplyDelete
  2. hawa jamaa wanatuchezea sana hivi tutawezaje kuwaambia kwamba tunachukia hali hiyo?

    ReplyDelete
  3. tunahitaji maarifa sasa,uhuru wa kweli ili tujitambue kwamba nafsi zetu ni zipi katika nchi hii

    ReplyDelete

Maoni yako