November 13, 2008

kipindupindu kiingie ikulu


sikujua uchungu, sononeko la moyo
akili yagota kwangu, moyoni harijojo
ghadhabu yanisibu,adhuhuri si kikomo
dibaji ya nini,uchafu mitaani?

kila leo twaumwa,vichomi na kuhara
miili yatuuma,akili nayo yagoma
maji haba salama, twanywa ya visima
dibaji ya nini uchafu mitaani?

kipindupindu chapindua,kinyesi kuwa maji
mwili kukongoroka,acheni dhihaka jamani
kila leo twanya uharo, ikulu vipi?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

kipindupindu ikulu,napenda kitinge
waharishe wakuu,nasi tupumzike
aghalabu isiwe vigumu, wanye uharo preeee
wakome na kuona mashudu,wanune au wacheke?
dibaji ya nini,uchafu mitaani

ngoja kipindupindu kiingie ikulu
ooooh alamsiki waungwana wema

No comments:

Post a Comment

Maoni yako