November 11, 2008
Je ni mapenzi yangu kuwa hali hii??
sijui jawabu, labda nimekosa thawabu
Hakika sina aibu, maisha ni yangu
Ni maisha yangu, ndiyo thawabu yangu
kamwe hiana si kwangu, nangoja adabu
Naishi kivyangu, siishi waishivyo
Moyoni furaha yangu, imani ilivyo
Furaha imedumu, haina kasoro
kuishi kudurusu, thawabu yangu
Salamu wenye heri, mola awarehemu
mioyo iwe buheri, nafsi zidumu
Moyoni sina huzuni,jirani usiniudhi
yangu yakuudhi, yako yanipa riziki?
Aghalabu sipigi kite, kwani mola ajua
mababu wasisikitike, moyoni natunza
imani isipotee, liwalo leo na kesho
faraja inikuze, upendo udumu hata mtondogoo
Wanipata ewe mwanadamu, sikio walitega?
akilize zidumu,ubongo wako umejaa
wanielewa ewe chakaramu, kesho unaogopa
sifazo ewe mwanadamu, itakupa malapa
ooh kwaheri ewe mnumanuma, ewe mpenda lukuma
alamsiki nakwambia, buheri na afya njema
sina hiana nakuga kwa pendo, iwe siku njema
siku ya upendo siyo mitego,iwe daima pamoja
Madhumuni
amani na upendo,
kumbukumbu,
maisha,
mapenzi,
mengineyo,
Nyasa,
urafiki
WASIFU: Mwandishi wa Habari,Tawasifu,Mhariri na Mchambuzi wa Vitabu,Siasa, Utamaduni, Michezo,Afrika, Kimataifa,Mshauri wa Habari na Mikakati. TUWASILIANE: mawazoni15@gmail.com, lundunyasa@yahoo.com. WHATSAPP; +255 719226293/SMS; +255 764 936655
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
inaonekana yeye atakuwa mchezaji mzuri wa mpira. Vumilia tu mwanangu ridhiki yako inakuja. Mvumilivu hula mbivu.
ReplyDeleteLabda maoni yangu yatokane na picha. Nionacho hapa ni CVHANGAMOTO ya maisha. Ambayo kama kijana hatoruhusu iharibu maisha yake ataweza kunyanyuka kimaisha na kuwa mfano kwa wengi. Labda niseme kuwa picha hiyo yawakilisha mamilioni ya waTanzania na waAfrika ambao wamenasa. Lakini ni kwa kuwa tunanasa akili kwanza, tunashindwa kujikomboa vema. Tukiamuwa tunaweza na kuamua ni kukubali kichwani kuwa tunaweza na baada ya hapo tutatumia kila kilicho ndani ya uwezo wetu kufanikisha mipango yrtu.
ReplyDeleteSi mapenzi ya Mungu kuwa katika hali hiyo, ila kabla hujamuomba Mungu akusaidie kuondokana nayo, jiulize "NINA MIPANGO GANI NINAYOTAKA MUNGU ANISAIDIE?" Mungu hatokupa mipango, ataiwezesha mipango yako.
Blessings
hapo sawa, kwani nikiitazama sana picha inanifikirisha sana inanipeleka mahali ambapo natakiwa kuwaza nahitaji nini katika maisha yangu.
ReplyDeleteKwa sasa hivi Obama anatia moyo watu kuwa kuna mambo yanawezekana hata ukitokea katika hali ambayo watu hudhania haiwezekani.
ReplyDeleteLakini Obama alikuwa na msaada angalau ulimpa msingi. Nivigumu sana kujikomboa ukiwa umesimama peke yako.
Picha hii inavuta tafakari kubwa.Laiti watengeneza sera wetu wangekuwa wanaguswa na taswira kama hii basi pengine wangekuja na maamuzi ya busara zaidi.Inasikitisha kuona kijana kama huyo pengine hajui mwaka ujao utakuwaje (pengine hata hana uhakika wa siku inayofuata).Ni rahisi kumpa moyo asikate tamaa lakini kwa hakika ni vigumu.
ReplyDeletemzee wa changamoto KARIBU SANA NYASA
ReplyDeletetuko PMOJA DAIMA
Asante sana Mzee wa Nyasa. Ni faraja kutua "nyasaland" na nashukuru kwa kunitembelea.
ReplyDeleteBlessings
nej inte alls det är synd om honom och det är inte snällt heller eler?
ReplyDeleteErik wa Sweden