November 11, 2008

Je ni mapenzi yangu kuwa hali hii??


sijui jawabu, labda nimekosa thawabu
Hakika sina aibu, maisha ni yangu
Ni maisha yangu, ndiyo thawabu yangu
kamwe hiana si kwangu, nangoja adabu

Naishi kivyangu, siishi waishivyo
Moyoni furaha yangu, imani ilivyo
Furaha imedumu, haina kasoro
kuishi kudurusu, thawabu yangu

Salamu wenye heri, mola awarehemu
mioyo iwe buheri, nafsi zidumu
Moyoni sina huzuni,jirani usiniudhi
yangu yakuudhi, yako yanipa riziki?

Aghalabu sipigi kite, kwani mola ajua
mababu wasisikitike, moyoni natunza
imani isipotee, liwalo leo na kesho
faraja inikuze, upendo udumu hata mtondogoo

Wanipata ewe mwanadamu, sikio walitega?
akilize zidumu,ubongo wako umejaa
wanielewa ewe chakaramu, kesho unaogopa
sifazo ewe mwanadamu, itakupa malapa

ooh kwaheri ewe mnumanuma, ewe mpenda lukuma
alamsiki nakwambia, buheri na afya njema
sina hiana nakuga kwa pendo, iwe siku njema
siku ya upendo siyo mitego,iwe daima pamoja

8 comments:

  1. inaonekana yeye atakuwa mchezaji mzuri wa mpira. Vumilia tu mwanangu ridhiki yako inakuja. Mvumilivu hula mbivu.

    ReplyDelete
  2. Labda maoni yangu yatokane na picha. Nionacho hapa ni CVHANGAMOTO ya maisha. Ambayo kama kijana hatoruhusu iharibu maisha yake ataweza kunyanyuka kimaisha na kuwa mfano kwa wengi. Labda niseme kuwa picha hiyo yawakilisha mamilioni ya waTanzania na waAfrika ambao wamenasa. Lakini ni kwa kuwa tunanasa akili kwanza, tunashindwa kujikomboa vema. Tukiamuwa tunaweza na kuamua ni kukubali kichwani kuwa tunaweza na baada ya hapo tutatumia kila kilicho ndani ya uwezo wetu kufanikisha mipango yrtu.
    Si mapenzi ya Mungu kuwa katika hali hiyo, ila kabla hujamuomba Mungu akusaidie kuondokana nayo, jiulize "NINA MIPANGO GANI NINAYOTAKA MUNGU ANISAIDIE?" Mungu hatokupa mipango, ataiwezesha mipango yako.
    Blessings

    ReplyDelete
  3. hapo sawa, kwani nikiitazama sana picha inanifikirisha sana inanipeleka mahali ambapo natakiwa kuwaza nahitaji nini katika maisha yangu.

    ReplyDelete
  4. Kwa sasa hivi Obama anatia moyo watu kuwa kuna mambo yanawezekana hata ukitokea katika hali ambayo watu hudhania haiwezekani.

    Lakini Obama alikuwa na msaada angalau ulimpa msingi. Nivigumu sana kujikomboa ukiwa umesimama peke yako.

    ReplyDelete
  5. Picha hii inavuta tafakari kubwa.Laiti watengeneza sera wetu wangekuwa wanaguswa na taswira kama hii basi pengine wangekuja na maamuzi ya busara zaidi.Inasikitisha kuona kijana kama huyo pengine hajui mwaka ujao utakuwaje (pengine hata hana uhakika wa siku inayofuata).Ni rahisi kumpa moyo asikate tamaa lakini kwa hakika ni vigumu.

    ReplyDelete
  6. mzee wa changamoto KARIBU SANA NYASA
    tuko PMOJA DAIMA

    ReplyDelete
  7. Asante sana Mzee wa Nyasa. Ni faraja kutua "nyasaland" na nashukuru kwa kunitembelea.
    Blessings

    ReplyDelete
  8. nej inte alls det är synd om honom och det är inte snällt heller eler?

    Erik wa Sweden

    ReplyDelete

Maoni yako