December 01, 2017

MACHO VITABUNI


NAAM! Mara kadhaa ninapotembelea jiji la Dar es salaam wengi hutuita  wageni kama “watu wa mikoani”. Lakini ninachokiona wakati mwingine ni kuzikali fursa ikiwemo ya kutembelea maduka ya vitabu.

Wahenga wanasema ni heri ukatekwa nyara, kushikiliwa mateka kwa muda fulani katika duka la vitabu kwani unakuwa umehiari mwenyewe. Pia wanasisitiza kitabu ni silaha. 

Siku hii nilitembelea Duka la Vitabu la TPH (TPH Bookshop) lililopo maeneo ya Samora, jijini Dar es salaam. Nilitumia dakika 45 kusaka vitabu mbalimbali. Waungwana nawaomba someni kwa furaha!

Katika ziara yangu nilivutiwa na kitabu cha Historia ya Wahadzabe. Nimekipenda, napenda kusoma vitu vinavyohusu Afrika na kama vinavyohusu dunia ujue ni vya sport. Mojawapo ni kitabu cha mwandishi Michael Dean kiitwacho “World Cup”, nilikisoma kwa masaa machache sana, sasa nimeweka kiporo kusoma Autobiography  ya Geoff Hurst pale  nyumbani. Nafikiri nilipokiona kile cha “Mbali na Nyumbani” nilitamani mno, nikaja kuachwa hoi na kile “WHY MEN LOVES BITCHIES” nilichoka looooh!
Ndiyo uhondo wa vitabu.

Wasalaamu watu wangu

Honorius Mpangala,
Kigoma, Tanzania

No comments:

Post a Comment

Maoni yako