November 02, 2017

KAMPUNI YA MKUKI NA NYOTA WAINGIA SOKO LA VITABU CHINA


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mkuki na Nyota ambayo hujishughulisha na uchapaji wa vitabu imetanua wigo wa soko lake la uchapishaji na utangazaji wa vitabu baada ya kusaini makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) la nchini China.
 
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa MNN, Mkuki Bgoya amesema kuwa wamesaini Makubaliano na Shirika la World Affairs Press (WAP) ya China kufanya kazi pamoja katika miradi mbalimbali ya kuchapisha na kuvitangaza vitabu ikiwa ni njia mojawapo ya kutanua soko la kampuni hiyo barani Asia.

Mkuki na Nyota ni kampuni mashuhuri kwa uchapaji wa vitabu ambayo ilianzishwa mwaka 1992 jijini Dar es salaam. Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Walter Bgoya ambaye alitumia uzoefu wake wa miaka 18 ya kuwa Meneja Mkuu wa Tanzania Publishing House. 


Tangu wakati huo imefanikiwa kuchapisha vitabu vya wanazuoni wa sayansi ya jamii,siasa,utamaduni,riwaya,tamthiliya,sanaa,vitabu vya watoto na taaluma mbalimbali kwa kiwango cha juu kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
 
 MUHIMU: Pichani ni Rais wa WAP, Ma Jinpeng, Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota (MNN) bwana Mkuki Bgoya na wadau wengine wa ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na WAP.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako