NA MWANDISHI WETU
VUMBI lililosababishwa na
sakata la mchanga wa madini maarufu kama MAKINIKIA limeitikisa tena kampuni ACACIA
ambayo inamiliki kampuni zinazochimba madini hapa nchini katika maeneo mbalimbali
kanda ya ziwa, baada ya vigogo wake wawili kulazimika kuachia ngazi mapema leo.
Kwa mujibu wa Taarifa rasmi
iliyotolewa na kampuni ya ACACIA imeeleza kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon
pamoja na Meneja wa Fedha, Andrew Wray wamejiuzulu nyadhifa, lakini wataendelea
kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu.
“Wote wawili, Brad na Wray
watabaki katika kampuni hadi mwishoni mwa mwaka katika kuhakikisha makabidhiano
ya ofisi yanakamilika. Brad anarudi kwao Australia kwa masuala ya kifamilia,
wakati Andrew anatafuta kazi nyingine. Kwa sasa Bodi inapenda
kutangaza kuwa imewachagua Peter Geleta, ambaye alikuwa Mratibu Mkuu, atakuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu. Jaco
Maritz, ambaye kwa sasa ni Meneja Mkuu, atakuwa Meneja wa Fedha wa kampuni. Uteuzi
huo utaanza rasmi Januari 1, 2018,” ilisema taarifa ya ACACIA.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako