May 15, 2009

"HAPPY BIRTHDAY MARKUS"


Hongera MARKUS HONORIUS MPANGALA, mwana wa nyasa umpendaye MALCOM X kila leo au JENERALI ULIMWENGU na JULIUS NYERERE, amani kwao watu hawa!
UPENDO UWE NANYI
Nashukuru baba na mama
Kwa kunileta hapa duniani
Nami najivunia kuishi ndani
Nashukuru sana wangu maanani
Kwani yupo nami kwa shida na raha
Kama machozi na majonzi naamini yanapita
Nashukuru ndugu waliopo hai
Na wale wasiohai, nawapenda kikweli
Upendo wangu, zaidi ya mshumaa
Nitawaangzia kwa uwezo wangu daima
Ningali nawajali, upendo usiopimika
Kwani ni tunu yake maulana
nawashukuru marafiki zangu nyote
Bila ninyi nikiri siyo mwenyewe
Najua imani yangu nimejaza kibaba
Naamini mola yupo nasi daima
Anajali,kutulinda na kutuhusudu
Ndiyo maana avumilia wetu utundu
Nawashukuru enyi wapenzi mlokuwa nami
Nawapenda kama amri ya mola
Kwani ni agizo la thamani daima
Nipo nanyi kwa mapenzi ya maulana
Nawashukuru maadui wote
Kwani mnanifanya niwe kama nilivyo
Bila ninyi sitokamilika, nawapa upendo
Mungu mkubwa.
Ni siku yangu ya kufurahia kuzaliwa kwangu, nashukuru wanablogu wote mliopo karibu nami. kwa pamoja tuseme waweke upanga au shoka au kufa ama kupona-mtaani tutabanana kwa pamoja tutafanikiwa kile kinachotakiwa kufanikiwa.
Na kwa yule mke/mchumba/mpenzi/demu n.k, ingawa nanua hujui kama wewqe ndiwe ninayekuhitaji. Labda hujui kama wewe ndiwe ninayependa uwqe demu/mchumba/mke wangu, lakini leo ujue ni siku yangu ya kuzaliwa.
Ingawa leo malaria yamenibana lakini nashukuru manesi ingawa wameshika matako yangu na kunidunga sindano. Najua kwa nia njema nitapona ndiyo maana ukichomwa sindano takoni unaambiwa poleeeeeee, ingawa nilisahau kumjambia ili nimwambia nami poleeeeee.
Najua kila mmoja anayozawadi yake lakini Koero Mkundi sijaona zawadi yako, unabifu na mimi au? Nashukuru Yasinta Ngonyani, zawadi yako nimeipenda sana1 daima tupo pamoja! OOOOhhh kwa wazee wangu nawaambia mjue mtoto wenu ni mwingi wa utani, mnivumilie ninaposema nesi amechezea TAKO langu. nadhani mnajua mambo ya kutaka uzima
LAKINI
atakayeweza anitunuku kitabu cha THE WORLD IS FLAT cha Thomas Friedman, nimtafuta hadi najamba. Mwenyewe ninacho mknoni JULIUS KAIZARI na CRYSTAL RAPTURE pia nakwenda duku la vitabu sasa kujinunulia zawadi. Bwaya, Kaluse,Kamala, na wengine naweka ..................................... ili ujaze jina lako kama nimesahau.
upendo daima, salama kwa mchumbangu usiyejijua kama ni wewe, naweka ........ andika jina lako

7 comments:

 1. Kaka. AMANI KWAKO. Nakutakia siku njema ya kukumbuka ulivyoambiwa kuwa ulizaliwa (maana najua huikumbuki siku hiyo. Lol) na pia nakutakia maisha marefu mpaka pale ambapo yataanza kuwa mateso, then uamue la kufanya.
  Unaombewa Daima na popote ulipo, USIPOTEE SANAAAAA. Ama uko shamba kama mie?
  Blessings to you and HAPPY BIRTHDATE

  ReplyDelete
 2. Nami nakutakia siku njema. Lakini hujasema una miaka mingapi:-(

  Koto kulya somba za mahele yatiubungula mahi. mwenga ha ha ahaaaaa

  ReplyDelete
 3. Heri siku ya kuzaliwa,
  Yaonesha sasa umekuwa,
  Salaam hizi watumiwa,
  Kwani mema twakutakia.

  Kazana tena heri kukimbia,
  Tulipo mwisho hatujafikia,
  Hadi siku itayowadia,
  Ambayo Mungu ataamua.

  Heri heri kaka nakuombea,
  Ila zawadi mi sijanunua,
  Kwani Yasinta hakunambia,
  Imekuwa vigumu kujua.

  Long live boy!

  ReplyDelete
 4. Happy birthday bro!

  Big up sana...kama umri wako unavyoongezeka basi upana wa akili na upeo wako uongezeke pia.!

  Enjoy your day.

  ReplyDelete
 5. Heri ya siku ya kuzaliwa,tunakutakia maisha marefu.Mungu akubariki sana!!!!!!!Enjoy your day.

  ReplyDelete
 6. ni jambo la kumshukuru mungu kuona siku zako za kuwepo katika sura hii ya dunia.

  Nakutakia kila la kheri katika kuadhimisha siku yako ya kuzawaliwa.Endelea kutumia muda wako katika kufanya mabadiliko chanya katika dunia yetu na kufanya mahala bora na pa usawa.

  tutafika tu Markus..Happy birthday

  ReplyDelete

Maoni yako