May 16, 2009

HAPPY BIRTHDAY MARKUS II

Nawashukuru wanablogu wenzangu, nawashukuru kwa kila namna yaani hadi chozi linadondoka, nawakumbuka zaidi ninyi kwani mnanifanya nijue kwamba wapo watu wanaonijali zaidi. Koero Mkundi uko wapi mziwanda wangu?, u hali gani huko mafichoni??????
Amini upendo mtamu
kama salamu tamu
kwakoFadhy wangu
Wanipa hamu hamu
Mtanga wangu, asante daima
Uso wapwita chozi,rabana ajua
Nionacho, u mwanamalenga
Hakika nakusujudia
Dhima yako idumu,milele
Maisha yangu kama tetere
Naishi bila kelele,nisonge mbele
U wapi koero wangu
U wapi pacha wangu
Kilio waona humu?
Nione kwa tonge au saumu.
Asante Changamoto, nipo mjini
jogoo la shamba mie,siwiki mjini
mtandaoni nipo,mjini nyingi dili
asilani sitokwacha,niamini
Nawasalimu kwa hamu
sina simile wala gubu
Nawapenda ninyi,mdumu
sijafunga kufuli,mlango u wazi
Jasho la majukumu, lakula muda bloguni
Wape hi Marekani na mashariki ya mbali
Waambie bongo twaishi mambo ni shwari
Asante Yasinta,kwa siku yangu
Kumbukumbu najivunia wangu
Usijali tupo sawi,tudumu
Asantedada weshi, ukarimu udumu
Usumbufu ulokubali,kunikirimu
Ahadi yetu itadumu,daima idumu
mungu mkubwa waungwana
Nimetembelea maduka ya vitabu pale Afrikasana kwa dada Weshi Lema kisha akanipeleka Mikocheni pale mtaa wa Regent, nikajipatia kitabu cha "PESA NA MAWE" kitabu kizuri nimekipenda, nashukuru kwa wote mliopo nami kwa kila dakika, kaka Simon mkodo Kitururu naamini tuko pamoja daima.
Nawashukuru nyote nawapendeni sana, hata kama sijakutaja najua hapa ................................. utaandika jina lako.
Dada Yasinta kwa kila dakika ya kunijulia hali na kujua siku yangu nashukuru sana. Digna, Manka na wengine. Nawapenda sana, upendo utadumu kama samaki na maji ingawa malaria yalinisumbua lakini sikuacha kwenda dukani kujinunulia kitabu. nitaandika kile nilichojifunza baada ya kwenda katika maduka hayo na ukweli wetu watanzania.

3 comments:

 1. ASANTE kwa kutukumbuka katika mashairi haya pia nimependezwa na musimamo wako wa kupenda zaidi kutafuta mafundisho mbalimbali kutoka katika vitabu.

  ReplyDelete
 2. Hongera kwa siku ya kuzaliwa kaka!

  Happy birthday to you bro! Ishi zaidi na zaidi uzidi kutupa mambo haya matamu!

  ReplyDelete
 3. Hongera Mkuu!Asante pia kwa kutukumbuka Mkuu!

  Tuko Pamoja!

  ReplyDelete

Maoni yako