December 04, 2017

UJENZI BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY WAKARIBIA

NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ujenzi wa barabara ya lami nzito toka Mbinga wilayani Mbinga hadi mjini Mbambabay Wilayani Nyasa unatarajia kuanza hivi karibuni. 

BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA RC MDEME
Mndeme amesema hayo wakati akitoa taarifa ya kufungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Novemba 29 mwaka huu, wiki iliyopita. 




Katika kikao hicho ambacho kimewashirikisha wabunge wote wa Mkoa wa Ruvuma, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Mstahiki Meya na Wenyeviti wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma na watalaamu wa barabara mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma, amesema ujenzi huo uko pale pale na mipango inakwenda kama ilivyopangwa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako