August 24, 2014

"CHANGAMOTO ZA KILIMO NA WAKULIMA - NYASA"


Na Vitus Matembo, Mbamba Bay
MBOLEA YA RUZUKU: Wakulima wengi wa Nyasa hawaitumii mbolea ya Ruzuku ya Serikali, na kuwaachia watu toka Mbinga kuja kuichukua. AJABU, Mtu akitumia na akapata mavuno mengi. Wanafikiria ni WIZI WA KISHIRIKINA.
UVIVU: Namnukuu Mkuu wa Wilaya, Mh.ERNEST KAHINDI, huwa anasema daima "Wakulima wengi ukanda wa Ziwa Nyasa ni Wavivu kwakuwa hufanya kazi kwa muda mfupi, yaani toka saa 12.00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi. Tofauti na maeneo mengne wanaotegemea Kilimo".
NYANYA TOKA NYASA HAZINA UBORA NA HUOZA MAPEMA: Wakulima wengi wanajitahidi kulima Nyanya ila kutozihudumia ipasavyo na madawa husababisha wafanyabiashara toka Nyasa kununua Nyanya toka Mbinga na Songea. Wakati Nyasa kuna mito na ardhi nzuri.

KILIMO CHA KOROSHO: Nakumbuka Meja Generali Mstaafu S.S.KALEMBO aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alihimiza sana Wanyasa tulime zao la Korosho kwakuwa ardhi ya Nyasa ni nzuri kwa kilimo hicho kama ilivyo Tunduru, Lindi na Mtwara. Ila sijajua tatzo nini?.

KILIMO CHA MIWA NA KIWANDA CHA SUKARI LUNDO JAMANI KIMEKUFAJE.

KILIMO CHA TUMBAKU SIJUI KIMEFIA WAPI KULE RUHEKEI.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako