November 16, 2017

MV NJOMBE INAVYOFUNGUA FURSA KWA WAKAZI ZIWA NYASA.


Honorius Mpangala, 0628994409

NA. HONORIUS MPANGALA
AKIWA katika kampeni za urais mwaka 2005 Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete katika ardhi ya Kyela Mkoani Mbeya alihaidi meli. Alirudia tena kauli hiyo alipokuwa katika ardhi ya Mbamba Bay Mkoani Ruvuma. Baada ya kipindi cha utawala wake hatimaye meli alizoahidi tayari zimeonwa na Wanyasa. 

MV Njombe imekamilika na kufanikiwa safari moja ya majaribio kutoka Bandari ya Itungi hadi Mbamba Bay.  Yapo mambo ambayo ni fursa kwa wakazi wa Nyasa kutokana Meli hii. Kama inavyoitwa ni meli ya mizigo ni chombo kitakachoweza kuwainua kiuchumi wakaza wa Nyasa kama watakitumika ipasavyo. Kuinuka kiuchumi kutatokana na kujikita katika shughuli ambazo wakazi wake watajishughulisha na shughuli kama ilivyo kilimo biashara na hata ufugaji wa kisasa na wenye tija katika maisha ya leo.
Kilimo cha biashara ni moja ya ujasiriamali ambao watu wengi wamekuwa wakijishughulisha nao. Katika mwambao wa Ziwa Nyasa hususani wilaya Nyasa yapo mabonde ambayo yanaweza kufanyika kilimo cha mazao ya muda mfupi na kwa mfumo wa kilimo cha umwagiliaji, na kile cha kutegema mvua na kuleta tija.


Meli yetu inahitaji mizigo ya kutosha. Kwa maeneo kama ya Liuli katika mashamba yaliyoko Nkalachi ni eneo ambalo ustawishaji wa mananasi na matikiti unaweza kuwa wenye tija zaidi. Maeneo ya Mango kuna uzalishaji mkubwa wa Manchungwa,machenza na mananasi pia. 

Bonde la Lundo ni eneo ambalo tangu zamani wakazi wa maeneo hayo walilima mahindi wakati wa kiangazi na hata mazoa kama miwa hulimwa. Bonde lile kama sio siasa basi Leo hii tungeona kiwanda cha utngenezaji wa sukari katika kijiji cha Lundo.

 Maeneo ya Ndesule katika mji wa Mbamba bay ndiko uzalishaji wa mpunga unakofanyika pamoja Taambachi. Katikati ya vijiji vya Kilosa,Likwilu na Linda kuna eneo ambalo hufanyika uzalishaji mkubwa wa mpunga karibu na Ndecha. Undu na Matenje wekuwa wakulima wakubwa wa tumbaku katika Bonde la mto Ruhekei. Zoole ni eneo maarufu kwa kijiji cha Chiulu katika kilimo cha mpunga. 

Maeneo ya uzalishaji yamekuwa mengi na makubwa hata Kwa ukanda wa Lituhi pia.Kama inavyofahamika vijiji vyake vyote vimekuwa vikilima sana zao la muhogo na kuwa la chakula. Lakini kupitia kilimo biashara unaweza kuufanya muhogo ukawa zao la chakula kulingana na watu wenyewe kama watataka kuyafikia masoko.

Ziko nchi za jirani zenye uhitaji mkubwa wa mazoa toka Tanzania. Tangu zamani wakazi wa Nyasa walisafirisha mihogo na mahindi kupeleka Malawi. Iliwahi kutokea wakati Jakaya Kikwete akiwa mgombea wa Urais alitumia mamlaka yake ya uwaziri wa mambo ya nje kuhoji juu ya Mizigo wa mahindi alioukuta Bandarini Mbamba bay. Swali lake alitaka kujua ni wapi mahindi Yale yanapelekwa,swali ambalo Said Kalembo aliyekuwa mkuu wa mkoa alishindwa kulijibu.
 
Moja ya makosa yanayifanyika Kwa wakazi wa Nyasa ni kuamini uvuvi ni shughuli pekee ambayo wanaweza kuifanya na kuwainua kiuchumi. Katika dunia ya sasa ambapo kila taifa lina pambambana kujiimarisha kiuchumi linahitaji watu wachapa kazi katika kufikia malengo ya kujiinua wao wenyewe na taifa Kwa ujumla. Baada ya shughuli za kilimo Kwa msimu wa masika ni vyema watu wakatambua wanahitajika kuendelea na kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yenye vyamnzo vizuri na vya uhakika vya maji.

Unaweza kuwa mzalishaji mzuri wa karoti, kabeji na hata tangawizi na kutafutiwa soko katika maeneo tofauti na yale ya uzalishaji. Meli yetu itahitaji mizigo kutoka maeneo mbalimbali na kufikisha sokoni mazao ya biashara. Kujikita katika shughuli za kila siku lazima kutapunguza ulevi uliokithiri wa Wanzuki na watu kutumia fursa ya uwepo wa meli ya mizigo katika kuzalisha na kifikisha mazao sokoni.

Kama ilivyo kwa wakazi wa maeneo ambayo reli imepita wamekuwa wakiitumia garimoshi katika kusafirisha mizigo na kufikisha sokoni. Ukiwa Morogoro ni rahisi kuona mizigo ya Asali ikishushwa katika kituo cha garimoshi. Ni asali inayotoka Kigoma na kusafirishwa hadi Morogoro. 

Pia Utaona Mikungi ya ndizi inashushwa maeneo kama Dodoma ikitokea Kilosa ambako imelimwa maeneo ya usagara. Watu wamekuwa wakitumia njia za usafirishaji katika kujipatia fursa na kujiinua kiuchumi baada ya kutambua wapi yaliko masoko.

Ni lazima tubadili mitazamo yetu katika kutambua tunahitajika kupambana ili kuinua uchumi wa maeneo yetu Kwa kufanya kazi. Nchi za Malawi na Msumbiji na hata nchi za maziwa makuu tunaweza kuzitumia katika kufikisha mazoa yetu na kufanya biashara na kutambua umuhimu wa kilimo biashara.

Yapo mazao ambayo hayajozoeleka sana katika ulimwaji wake na ni mazoe yenye tija. Mazao kama ya Tangawizi, Karoti na hata Ufuta ni mazao ambayo watu wanaweza kulima na kufanikisha soko la mazao hayo kutambulika ni wapi hupatikana. Ili kufanikisha biashara ya mazao ambayo itafanya meli ya mizigo kupata mizigo ya kufikisha katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa wa kufanya biashara.

Raha ya hii meli itakuwa nzuri sana kama itapita katika vituo vyake kama vya Lundu, Mkili, Nsinsi, Ifungu, Rumbila, Lupingu, Manda Njambe na kupakia mizigo ya kutosha na kufikisha maeneo mengine kwa ajili ya kufikishwa sokoni.
0628994409

No comments:

Post a Comment

Maoni yako