NA.
HONORIUS MPANGALA
0628994409
ILIKUWA
miaka Sita ya Ubabe wa soka barani Afrika kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Kila
mpenzi wa soka alimfahamu Hassan Shehata,kila mpenzi wa soka alimfahamu Waile
Gomaa. Ilikuwa nyakati za Misri kunyanyasa mataifa mengine ndani ya bara la Afrika.
Ilimchukua Kameruni miaka tisa kulipiza manyanyaso aliyopata toka kwa Misri ya
kiumeni mwaka 2008 pale Ghana.
Ni
Misri ambayo iliipa hasara CAF kuunda kombe lingine la Afcon baada ya kulibeba
lile awali Mara nne Mfululizo. Mwaka 2006 fainali zilizoandaliwa na Misri
wakikutana na Ivory coast ya Didier Drogba.
KIKOSI CHA MISRI |
Fainali
ile iliisha kwa matuta na wenyeji kutwa taji. Licha ya kuwa na kikosi ambacho
kilikuwa na vijana taklibani Saba wakitoka kikosi cha Al Ahly ambayo ilikuwa
moto wa kuotea mbali. Hapa
nawazungumzia Mohammed Barakat,Saeed Moward,Essam El Hadary,Ahmed Hassan,Hossam
Hassan,Mohammad Mido,Mohammed Aboutrika na wengineo. Ilikuwa ni kikosi
kilichojaa vipaji kikiwa na hamasa kubwa kutoka kwa kocha mzawa Hassan Shehata
kiliwafanya wapinzani wafikirie Mara mbili zaidi.
Ukuta
ulioongozwa na Waile Gomaa ilikuwa kama unakutana na Rio Ferdinand wa nyakati
za Vodafone na Manchester Utd yake. Beki mmoja chuma halafu bedui anacheza
kibabe kiasi kwamba hupati nafasi ya hata kumiliki mpira kama mshambuliaji. Kwa
lugha za sasa za mtaani unaweza kusema 'ana kuvugaa' kama ulivyo.
Si
mnakumbuka Zengwe la Hassan Shehata na Mido katika Nusu fainali ya afcon iliyowalutanisha
Misri na Senegal 2006. Ilikuwa Senegal ya vipaji haswa. Kuna nyakati unaweza
kukaa na kutoa majibu kuwa soka la kipaji limeondoka miguuni mwa wachezaji
tunao watazama sasa.
Lile
zengwe ilikuwa baada ya Kufanyika mabadiliko yaliyomuingiza uwanjani Amri Zaki
na kumtoa Mido. Mwarabu yule hakufurahishwa aligombana kwa maneno na kocha
wake. Ajabu ya mwenyezi Mungu Zaki akafunga bao lililowapeleka fainali na
kumwacha Mido akishindwa kushangilia huku Shehata akimwonyeshea kidole katika
kichwa chake akimaanisha akili.
Licha
matukio matamu yenye kusisimua kwa nyakati za zote za Ubabe wa Misri jambo
pakee ilikuwa kizazi hicho hakikufanikiwa kufuzau kombe la dunia. Asikudanganye
mtu hakuna raha kama kuimbiwa wimbo wa Taifa katika mashindano ya kombe la dunia.Misri
walijaribu kuitafuta raha hiyo lakini wakaishia kuipata wanapocheza Afcon.
Mara
ya mwisho kwa Misri kushiriki ko be la dunia ilikuwa mwaka 1990. Katika fainali
zilizofanyika nchini Italia ikawa mwisho wao hadi sasa ambapo Mohammed Sarah
anawapeleka Urusi mwakani. Ilikuwa nyakati za utawala wa Hosney Mubarak ndipo
waMisri walipoimba kwa pamoja na wachezaji wao wimbo wa taifa pale Italia.
MOHAMMED SALAH |
Wakiwa
na nahodha na golikipa mkongwe Essam El Hadary Misri wanafuzu huku akiwa na
wadogo zake ambao wametengeneza kikosi kilichoandika historia ya Misri tena.
Matumaini ya kurudi katika Ubabe wa soka la Afrika yalianza kuonyesha matumaini
katika michuano ya Afcon ya mwaka huu pale Gabon. Ukikitazama kikosi chao kina
majina maarufu mawili yaani Mohammed Sarah na Mohammed Elneny katika dimba huku
kaka yao El Hadary akihakikisha hakuna mpira unaompita na kutinga wavuni.
Juni
8 ilikuwa ya kihistoria kwao baada ya kufanikiwa kutinga faninali za kombe la
dunia la mwakani. Magoli ya mawili ya Salah dhidi ya moja la Congo Brazzaville
yaliwapaisha na kuwafikisha Urusi.
Jambo
pekee katika Mchezo huo ni goli la dakika ya 90+3 lililofungwa kwa mkwaju wa
penati na Salah ndilo lililofanya Misri yote ilindime kwa Shangwe vifijo na
ndelemo. Ilikuwa zaidi ya sherehe kila mmoja alijikuta akifurahia matokeo ya
Timu ya taifa licha ya tofauti za kisiasa zinazolitafuna taifa hilo kwa
maandamano na mapigano ya wanajeshi wa serikali na Waasi.
Ukitaka
kujua raha ya kuimbiwa wimbo wa taifa kombe la dunia muulize Serey Die nahodha
wa sasa Ivory Coast. Alitoa mchozi wakati wimbo wa taifa unaendelea pale Brazil
katika Mechi iliyowakitanisha Ivory Coast dhidi ya Japan. Mchezo ambao wapenzi
wengi wa soka ilibidi wasubili hadi kumi za usiku kwa masaa ya Afrika mashariki
kumwona Die akiangua kilio.
WAEL GOMAA |
Nawaona
wamisri wakiangua kilio zaidi ya kile walichoangua pale Misri baada yachezo
dhidi ya Congo Brazzaville. Ilikuwa kama ndoto kwa mkongwe El Hadary kutimiza
ndoto za kuisaidia Misri kufuzu kombe la dunia. Vilio
vya uchungu walivyolia Wamisri pale Sudan mwaka 2009 vimegeuka vilio vya furaha
kwa mwaka 2017. Kuna wakati mnaweza kupitia mitihani mikubwa lakini kumbe Mungu
anakuwa na maksudi nanyi.
Ubabe
wa Afcon kwa wamisri haukuwapeleka kombe la dunia lakini unyonge wao wa wakati
huu unawafanya watimize ndoto na kwenda kuimba wimbo wao wa 'My country' katika
ardhi ya Urusi. Utamu wa wimbo wa taifa mchezaji auimbe akiwa kombe la dunia.
Hakuna
hoja yoyote ambayo inaweza kumfanya mtanzania akaona kama ni ya kujifunza Kwa
kufuzu Kwa misri. Kama kufuzu Kwa Serengeti watanzania walichangiani je kwa Taifa
Stars? Unajisikiaje Rais wa Misri kamwaga pesa Kwa vijana wake au unasikia Rais
wa Panama kaamua siku moja kufanyika mpumziko ili kuwapongeza vijana wake.
Misri
mmepata mlichokitafuta kwa miaka takribani ishirini na sita. Nendeni Urusi
mkawakilishe Wafrika ambao watakuwa wanawachukulia kama timua yao.
0628994409
No comments:
Post a Comment
Maoni yako