October 11, 2017

MTAHINI ANAPOKUWA MTAHINIWA.

NA KIZITO MPANGALA
Nchini Nigeria zaidi ya walimu 20,000 kufutwa kazi kutokana na "hat trick" iliyofanywa na serikali ya nchi hiyo kwa kuwatahini walimu mitihani ile ile ambayo huwa wanawatungia wanafunzi wao.


 Walimu zaidi 20,000 wamafeli mtihani huo hali ilinayofikirisha wengi kuwa inakuwaje mtahini ashindwe utahiniwa? Hivyo, uamuzi wa serikali ya Nigeria ni kiwafuta kazi wale wote ambao wamefeli mtihani huo.

Hilo linanikumbusha mwaka 2011 ambapo mwalimu mmoja wa Seminari ya Likonde nchini Tanzania alitoa simulizi fupi kuhusu mchakato na manyanyaso waliyokuwa wakipata msimu wa kusahihisha mitihani ya kitaifa ambao ulikuwa ukifanyika jijini Dar es Salaam. 

Viongozi wa wizara ya Elimu pamoja na wale wa baraza la mitihani wakati huo walikuwa wakiwataka walimu wanaokuja lusahihisha mitihani hiyo watahiniwe kwanza ndipo wajue nani anafaa kusahihisha. 

Walimu wote kwa ujumla walitoa pendekezo kwamba wao waanzr kuwatahini viongozi wote wa wizara ya elimu na baraza la mitihani mtihani uleule uliofanywa na wanafunzi wao ndipo wajue kama wanafaa kusimamia Elimu nchino. Hapa hapakitosha kabisa! Hakuna aliyetaka kuaibika!

Hivyo basi, Nigeria wameua lufanya hivyo na wamewanasa waliowataka. Taifa la Nigeria lina watu wengi sana barani Afrika hivyo utoaji Elimu una changamoto kubwa. Hali hii imeilazimu serikali kuruhusu shule nyingi binafsi kianzishwa kwa ada elekezi.

RAI:
Lengo siyo kuwaaibisha walimu, lengo ni kujua nani ni nani katika nini. Hilo siyo mbafala wa vyeti feki. Hivyo, ingawa kuna maswali Mengi ya kuuliza kuhusu jambo hilo, ni vema walimu wawe na utamaduni wa kuperuzi vitabi mbalimbali kulingana na somo husika analofundisha ili kujiimarisha katika ufahamu na kuweza kiwapa wanafunzi kinachostahili. 

Pia serikali iongeze ubora vitabu na kuchapisha vingi na ikibidi hata vitabu vya ziada viruhusiwe kwa kuwa vipo vingo vizuri na bora. Na jambo la mwisho ni kuwajali walimu. Si tu yule anayeitwa profesa ndiye anastahili kujaliwa, bali yeyote aliye mwalimu anastahili hilo. Na walimu wenyewe wajielewe kuwa wao ni walimu.

©Kizito Mpangala

No comments:

Post a Comment

Maoni yako