December 27, 2008

karibu nyumbani Yasinta, nina HAMU

duuuh unajua kwanini huwa naandika sana kuhusu huyu mtu? usiulize wewe pigia tu mistari au vipi. Ni jambo jema sana kukukaribisha tena nyumbani,kunyumba, hakika ni raha sana. Nashukuru pia kwa muda wote ambao umetumia katika shajara/blogu yako maana kuna kipindi ulikuwa katika mawazo sana kama siyo MAWAZONI, ndiyo maana nilisema nitafungua MASHTAKA iwapo ungeacha kublogu. Leo nafarijika namna unavyofanya kazi njema na kuibua mada motomoto ambazo hufikirisha. Hata hivyo naamini kutokuwapo kwako hewani ni kwa muda mfupi nina hakika na naamini utarejea tena baada kula DAGAA NYASA weeeeeeee karibu kunyumba bambu likolo la manyungu, mbulika, magege,kitimoto,ULANZI, komoni, myakaya na mambo mengi sana. Karibu nyumbani jamani maskani palipali pa mfaranyaki au kubombambili mmmm kuruhuwiko kwa Matetereka? haha ha ha nina raha sana maana nyumbani ni nyumbani, wale DAGAA wamefanya kazi sana maana najua mate yamekujaa mdomoni leo. KARIBU NYUMBANI dada Yasinta lakini kumbuka mashtaka yangu ukiacha kublogu tu yapo palepale!!! Erik a.k.a spite boy + Camilla a.k.a baby boom karibuni nyumbani. PAMOJA DAIMA

8 comments:

 1. Asante sana Markus tayari nimeshafika.

  ReplyDelete
 2. Karibu sana. Mungu akutangulie.

  ReplyDelete
 3. asante sana Fadhy nakuja yaani raha kweli

  ReplyDelete
 4. Markus una hamu ya nini? sijakuelewa je unaweza kuniambia au kutuambia. ha ha ha ha haaaaaaaaa

  ReplyDelete
 5. haya ndugu yangu nimefurahi zaidi nakuomba tuwasiliane zaidi ili tufahamishane mengi

  ReplyDelete
 6. Yasinta wakati mwingine anapenda sana uatni lakini ukimtania bila kuwa makini utaona vijambo ha ha ha eti anauliza nina HAMU ya nini hoo kwani miye siye binadamu nisiwe na hamu ya kuonana wenzangu. mmm unajua ndiyo maana umemaliza kwa kucheka ha ha ha ha ndiyo nina HAMU sana tu nimekumiss au vipi mwanawane

  ReplyDelete
 7. Hata mimi nilikuwa najiuliza hamu ya kunywa chai na samaki, au? nadhani hivyo.

  ReplyDelete

Maoni yako