February 04, 2009

Rahaaaa sanaaaaa

Sijui labda unatupenda ila husemi.

Pengine unaweza kutuambia lolote, unaweza kutafsiri chochote lakini sisi ni kama wewe, tupo pamoja nawe daima! Vipi unawaza nini utuonapo, au kuna lolote unajifunza? Tulia mwenzetu ule kwa raha, usafiri kwa raha wala usitie shaka, kwani ile gari yako unaweka mafuta lita ngapi na kwa shilingi ngapi?
Maana hapa tunakula kwa dola moja siku nzima. Si unaijui BUKU au elfu moja, wenzio tunatumia kwa siku mpaka inabaki kwaajili ya kesho, siku ambayo tutaongezea nyingine ili itimie kama ile. Tunafurahi, tunaridhia maisha yetu, wala hatutaki kukaa eneo lenye maandishi '"mbwa wakali" au "eneo hili linalindwa kwa mitambo maalumu".
Wala kwetu hatuna walinzi tuwalipao kwa miezi 12. Pengine unadhani siye wanyonge! unajidanganya, tunauwezo kuliko wewe unavyodhani, tunaweza kutenda na kuenenda kama wewe lakini tumetulia kwa raha na tabasamu utuone kwanza! Vipi unaonaje!

No comments:

Post a Comment

Maoni yako