February 03, 2009

Ukishiba, msome Richard Wright

Kama utashiba bila mboga au kama imekwisha basi msome Richard Wright maneno yake haya " Hatari inayoukabili ulimwengu wa leo ni kusahau kile kiainishacho ubinadamu wetu. Maana halisi ya mahusiano, maana halisi ya mapenzi, hata ile heshima na hadhi ya maisha ya binadamu inaelekea kusahaulika. Kipimo cha utu si utu tena bali mienendo na tabia za kikatili na ufisadi.
Leo hivi mapenzi ni neno lililobadilika maana yake, sasa mapenzi ni uhusiano wa mtu na gari au mali yake.
Neno utu limebadilika kabisa maana yake na kuwa utukufu na ubinadamu ukawa ubwana damu hata damu imekosa thamani ya asili na utakatifu!

2 comments:

Maoni yako