May 23, 2013

SHAIBU NNUNDUMA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA WILAYA YA NYASA

Na Hoops Kamanga, Mbamba Bay
Halmashauri ya Wilaya mpya ya Nyasa imepata mkurugenzi wake ambaye atasimamia shughuli za wilaya hiyo. Mkurugenzi huyo ni Shaibu Nnunduma, ambaye ni Afisa Kilimo kitaalamu, ameteuliwa kuongoza wilaya ya Nyasa baada ya kufanya kazi wka ufanisi mkubwa alipokuwa wilaya ya Mbinga.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa, Ndugu Shaibu Nnunduma alikuwa mkurugenzi wa wilaya ya Mbinga. Shaibu Nnunduma alikuwa Mkuu wa Idara ya kilimo Masasi kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Bukoba kisha akapelekwa wilaya ya Mbinga.

Nnunduma ana shahada ya kwanza na ya pili za kilimo ni mwenyeji wa mkoa wa Lindi. Anasifika kwa kufanya mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo katika wilaya ya Mbinga kwa muda aliofanya kazi wilayani humo. Mojawapo ni ujenzi wa barabara za lami katika mitaa na uwekaji wa taa za barabarani na sasa ujenzi wa stendi ya kisasa mjini Mbinga.
PICHANI; Shaibu Nnunduma akizungumza na wakulima kuhusu namna bora ya kilimo cha kisasa.

2 comments:

  1. Hongera wanyasa wenzangu kwa kupata mkurugenzi mpya.Na twakutakia kazi njema.

    ReplyDelete
  2. Asante sana na tunaamini tutasonga mbele katika gurudumu la maendeleo

    ReplyDelete

Maoni yako