November 13, 2017

HEKIMA ZA AFRIKA KATIKA MISEMO.

Kwenye mabano ni sehemu ambayo misemo husemwa.

1. Usiku una masikio. (Masaai)
2. Adui mwenye ufahamu ni bora zaidi kuliko rafiki asiye na ufahamu. (Senegal)
3. Sufuria bora haitoi chakula. (Nigeria)
4. Hata simba, mfalme wa nyika, anajilinda dhidi ya inzi. (Ghana)
5. Kama kitendea kazi chako ni nyundo pekee, kila tatizo kwako ni msumari. (Gambia)
6. Aogaye maji ya baridi majira ya baridi kwa kupenda, hahisi baridi. (Ufipa)
7. Inzi wanaweza kumsumbua simba zaidi kuliko simba awezavyo kuwasumbua nzi kwa mkia wake. (Kenya)
8. Kifo cha mzee ni sawa na maktaba inayoungua moto. (Ivory Coast)
9. Ukiwa unatengeneza meza halafu msumari ukapinda, utaacha kutengeneza meza au utabadilisha msumari? (Rwanda)
10. Huwezi kujenga nyumba kiangazi kilichopita. (Ethiopia)

© HAZINA YA AFRIKA.
Na Kizito Mpangala.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako