November 10, 2017

MAJIMAJI FC KUFANYA ZIARA NYASA

 Na Mwandishi Wetu
 
KLABU ya Majimaji ya mjini Songea inatarajia kufanya ziara ya kimichezo katika wilaya ya Nyasa. Katika ziara hiyo Majimaji wanatarajiwa kucheza 
mechi mbili za kirafiki, Novemba 11 na 12 wilayani hapa. 

Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Mbamba Bay United na mechi ya pili dhidi ya Mkali Stars. Mechi zote zitapigwa katika dimba la Mkali. Mashabiki na wapenzi kutoka maeneo yote ya karibu na Mkali yaani kuanzia Kibagara, Mango, Songambele, Ngehe, Yungu, Nkalachi, Puulu, Liuli, Hongi,Maporomoko,Mkali, Lipingo, Lundo, Ngindo, Chinula, Ndengere, Mbamba bay, Kilosa, Likwilu. 

Kama unapata nafasi karia ndinga hadi Pale Mkali fika maeneo ya JB mapemaaa kusubili kuwaona Wanalizombe. Wameamua kuja kupata mitipitila ya kinyasa kabla ya kucheza na Mbao FC tarehe 18 mwezi huu.
Karibu Nyasa Wanalizombe huku dagaa na samaki Kwa ugali wa mihogo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako