December 05, 2008

alaaah! sina kipaji cha kupenda, sikujua hayo

Aghalabu ni ningelijua lakini hakika sijijui labda kwakuwa sijui ndiyo maana nipo hivi. Nakupenda ndiyo maana nilikuja mbele ya wazazi wako, ingawa hawajui wanajua sisi tunafahamiana na marafiki. Sasa kivipi ilikuwa vile jakamoyo ukaijenga ulikuwa ukighadhibika? mbona hukusema, ingawa mara chache ulinena? hukusema kama unajua sina kipaji cha kupenda sasa mbona najua hilo kama sina kipaji? Poa sina simile wala sipigi kite kwani najua WARINA asali hawajui utengenezaji wake, wao HURINA tu hawajui mweka SEGA ni nani. Sasa najua sina kipaji cha kupenda unatakaje? nitembee kama nani, niige za ughaibuni hapana! tena thubutu bwana. Sasa nifanyeje ingawa najua kwamba unanipenda lakini ile tarehe milele sitoisahau daima itakaa moyoni kama simanzi ulotaka kunipa. Dunia ni nini? mbona wanipa majonzi huku wajua nakupenda? Nashukuru umenisamehe lakini swali langu, KUMBE SINA KIPAJI CHA KUPENDA? alaah kwanini hukuninong'oneza? mbona ulikuwa kimya ukadai wanipenda, nashangaa hata mungu anatakaa kujifanya muumini wakati una zigo la madhambi? au kujiona bora mapenzini, acha dhihaka, kweli ndivyo nilivyoumbwa siwezi kujibadili au nisake kipaji kama RONALDINHO maana wahenga walisema WA MBILI HAVAI MOJA au tusemeje AOMBAYE KIGAE AWE NA CHAKE? sijui ila asante kunisamehe ingawa niliuchukia mwezi Novemba. Alaaah kumbe sina kipaje cha kupenda?????

2 comments:

  1. Naona sasa kaka Fadhy Mtanga umenisoma, sasa umenielewa. salamu kwa wote wanaonisoma amani iwe nanyi upendo uwe nanyi. NAMUOMBA MOLA ATUWEKE HAI DAIMA

    ReplyDelete
  2. Alaah kumbe una kipaji cha kuandika mashairi pia. Safi sana nimelipenda sana shairi lako endela kuandika mengi ya aina hiyo.

    ReplyDelete

Maoni yako