May 24, 2009

NYASA DEVELOPMENT ORGANISATION

Nilikuwa nimebanwa kidogo na semina za Freddy Macha, nikashindwa kuandika hapa, lakini nashukuru mungu nimerudi tena.
Ndugu zangu kimsingi jumuiya yetu hii ya Nyasa development organisation inaundwa na sisi vijana ambao kwa wastani kwa umri ni chini ya 27, tupo katika masomo tofauti kuanziia sheria, siasa, ustawi wa jamii, elimu, sanaa, kompyuta, na mambo mbalimbali yanayohusu elimu yetu.


Mradi huu ni ubunifu wetu kwamba kwa kiasi gani tunaweza kuibadili hali ya nyasa au maeneo yaliyopo katika jimbo la mbinga magharibi? hili lilikuwa swali kubwa sana kwetu, lilikuwa jukumu ambalo kama wanadamu tunapaswa kukabiliana nalo. kundi letu linaundwa na wanafunzi toka chuo kikuu cha dodoma, dar es salaam, IFM, na vingine vingi tu. kwani dhamira yetu ni kuwakusanya wenzetu ambao hawakuhudhuria awali tunaamini kuwa mchango wao ni muhimu sana,


Leo ni kikao cha pili, mazimio yatafikiwa na nitayaweka hapa. Tukumbuke huu ni mradi wa kujitolea, tumeamua kutumia nafasi tuliyopewa katika elimu na nchi yetu ili kuyabadili mazingira yetu. Mara nyingi namkumbuika sana Ndesanjo Macha, huwa nasisistiza kuwa ukitaka kuleta mapinduzi katika nyanja za kimaendeleo basi anza mwenyewe kwa kubadili sura ya mtaa wenu. Hilo ndilo lengo letu sisi vijana, maana tunaamini ni jukumu letu kuyaweka mapinduzi ya maendeleo katika ukanda wetu na hakika tuna dhamira kubwa sana, pia blogu yangu itakupasha mambo yote yanapohusu mradi huu na ikibidi kuanzisha blogu nyingine kama kutakuwa na umuhimu huo tutafanya hivyo mara mradi huu ukikaa ukiwa katika mhimili wake.


Nashukuru maoni ya mzee wangu Prof Mbele, kwa hakika umenipa faraja kubwa na kuona kwamba wapowatu wanaojali hali za wengine katika maisha. TUMEAMUA KWA DHATI, NA LEO HII NINAVYOANDIKA HAPA KUNA KIKAO KINGINE ILI KUIPANGA MIKAKATI ENDELEVU. tunakaribisha mawazo yenu ni muhimu sana.
kama unapenda kuwasiliana moja kwa moja na kiongozi wetu AMBROCE NKWERA, simu yake ni hii hapa 255-712514078, mawasiliano mengine tutayaweka hapa au niandikie katika barua pepe, lundunyasa@yahoo.com au jikomboe@gmail.com .
Leo ni kikao cha pili saa tisa katika ukumbu wa NewVenus pale mtaa wa Relini Tataba jirani na ofisi za gazeti la Mwananchi. KARIBUNI

1 comment:

  1. Kweli ni changamoto nzuri sana ni jambo la busara. Tupo pamja na tutafika tu.

    ReplyDelete

Maoni yako