November 20, 2012

SHULE YA MSINGI NDONGA YAHITAJI MATENGENEZO YA HARAKA SANA WILAYANI NYASA


Pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi NDONGA. Shule hii ipo katika hali mbaya sana kutokana na wanafunzi kusomea kwenye majengo mawili ya shule hiyo ambayo yaliezuliwa na kubomoka kutokana na upepo mkali mapema mwaka jana(2011). 
Eneo la Ndonga linajulikana kutokana na kukabiliwa na upepo mkali sana hasa kipindi cha kiangazi na masika. tangu kuezuliwa kwa paa la shule hiyo wanafunzi wamekuwa wakisoma huku wakipigwa na jua kali kutokana na kutoezekwa. 
Wanafunzi kama wanavyoonekana pichani hawanjakingwa na jua hivyo kuzorotesha ufanisi wao maishani. Ni Jukumu la wakazi wa kijiji cha Ndonga, Uongozi wa kijiji, Tarafa, na Wilaya ya Nyasa kushughulikia suala hili. 
Hali kama hii haiwezi kwuachochea wanafuzni kuwa wavumbuzi au wenye kiu ya kupata elimu kama maeneo mengine yenye mazingira mazuri ya kusomea kama Shule ya msingi Mwongozo iliyopo mjini Liuli. 
Mazingira kama haya yanampa wakati mgumu sana mwanafunzi kuweza kufanikisha ndoto zake, ndio maana wengi wanaishia kuwa watoro shuleni. jambo jingine ni kwamba mazingira kama haya ynachochea wanafunzi kutoona umuhimu wa elimu kwani mazingira wanayotumia hayatoa motisha ya wao kupenda shule. 
Shime watu wa Ndonga, uongozi, tarafa na wilaya yote ya Nyasa, ni wakati wa kushughulikia hili kwa kupitia watu wote wanaohusika katika kuboresha elimu yetu. Hali hii inawarudisha nyuma wanafunzi na walimu wao. 
Ili kuondokana na ukosefu wa walimu katika shule nyingi za Wilaya ya Nyasa hatuna budi kuhakikisha tunatengeneza mazingira mazuri ya wanafunzi na watoto wetu.

Picha ya Jamii Forum, kwa hisani ya Weston Ndomba, Nyasa

No comments:

Post a Comment

Maoni yako