Mvuvi akiwa na zana zake za kazi.
PICHA: kwa hisani ya kaka Francis Godwin
UHABA wa samaki ziwa Nyasa upande wa Tanzania unaochangiwa
na vifaa duni vya uvuvi umepelekea baadhi ya wanaume wa tarafa ya Mwambao
wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kutelekeza familia na kwenda nchini Malawi
kufanya shughuli za uvuvi kama njia ya kukwepa changamoto za uchumi
zinazoendelea kuwa kikwazo katika wilaya hiyo.
Uchumi wa wananchi wa tarafa yaMwambao ambao ulikuwa
ukitokana na ajira ya uvuvi kwenye ziwa Nyasa nao umezidi kuporomoka kwa kasi
kubwa na kupelekea hata biashara za wananchi wa maeneo hayo ambazo zilianzishwa
kutokana na wingi wa wageni waliokuwa wakifika kujumua samaki kwenye ziwa hilo
pia kuathirika kwa kiasi kikubwa.
Kama inavyofahamika kuwa uvuvi wa samaki kwa wananchi wa
tarafa ya Mwambao wilayani Ludewa ndio shughuli kubwa ya kiuchumi ambayo
imekuwa ikitegemewa na karibu robo tatu ya wakazi wa tarafa hii ya Mwambao na
ndio shughuli iliyopelekea tarafa hiyo kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha hasa
kipindi cha nyuma japo kwa sasa imeanza kubaki historia pekee.
Bonyeza kiungo; SOMA ZAIDI HAPA
No comments:
Post a Comment
Maoni yako