Shirika la Mindset Empowerment waandaaji wa mashindano ya
RUAHA MARATHON inawashukuru wasimamizi wa shughuli zake kwa upande wa DAR ES
SALAAM, Markus Mpangala na Kambi Mbwana, pamoja na akina dada waliojitokeza
kuwania nafasi ya kazi pale Mlimani City, Dar es Salaam.
Nimepewa taarifa kuwa
walijitokeza kwenye interview ni mabinti zaidi ya 50 na wamechujwa na
kupatikana mabinti watano (5) ambapo mmoja kati yao atachukua nafasi hiyo na wanne
kuwa reserve kwa majukumu mengine ndani ya Ruaha Marathon. Tunayo furaha
kutangaza tena nafasi 20 za kazi za kujitolea (volunteers) kwa vijana wa KIUME
na wa KIKE kwa ajili ya kufanikisha mashindano haya tarehe 25/May/2013, mkoani
Iringa.
ENEO LA KAZI: Iringa mjini & Iringa vijijini, kwenye
njia (route) za mashindano
MAJUKUMU: Kufanya kazi katika vituo vya marathon siku hiyo
ya mashindano
UKOMO: Kazi hii ni ya kujitolea kwa siku moja TU (siku hiyo
ya mashindano)
SEMINA: Wiki moja kabla ya siku ya mashindano kutakuwa na
semina kwa volunteers wote, kwa ajili ya ujuzi wa kufanikisha majukumu yao.
FAIDA: Pamoja na posho (allowance) atakayopewa volunteer
siku hiyo, vile vile atapewa cheti cha kimataifa kinachoonesha kujali, uzoefu
na ushiriki wake katika miradi ya kijamii (Ikumbukwe kuwa Ruaha Marathon
inafanyika mwaka huu kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule na kituo
cha michezo kwa watoto walemavu, Tanzania). Volunteers wote watakuwa ni watu
wanaofikiriwa kwanza (first priority) kila zinapotoea nafasi za kazi za kudumu
katika Shirika la Mindset Empowerment.
VIGEZO: Yeyote anaependa kuwa volunteer anatakiwa awe anajua
kungea na kuandika lugha ya kiingereza kwa ufasaha. Pia awe na ufahamu mzuri
kuhusu mambo mbalimbali. Wafanyakazi pia Wanafunzi & wahitimu wa vyuo
vikuu/vyuo mbalimbali na wengineo wanaoweza kufika, waliopo/au wenye makazi
Iringa mjini wanahamasishwa wasipitwe na fursa hii adhimu
KUTUMA MAOMBI: Tuandikie email: nyalukemarathon@yahoo.com au
tuma sms au piga katika +255 719 127 901. Unapoandika/kutuma sms zingatia: 1)
Andika majina yako yote matatu, 2) Elimu yako/mahali unaposoma au unapofanyia
kazi. 3) Umri wako 4) Jinsia yako. Baada ya kukutuma maombi yako; tutakujulisha
hatua inayofuata. Maombi tunaanza kupokea leo tarehe, 17/March/2013
IMETOLEWA NA: Albert Nyaluke Sanga, Mratibu-Ruaha
Marathon/Mindset Empowerment, 2013~(C)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako