Wataalamu
kama Robert Merton waliwahi kusistiza umuhimu wa uhalifu katika jamii. Lakini
kwa wataalamu hao hao wanasema, ikiwa njia za kujipatia pato zikibanwa au
zikibinywa uhalifu ni kitu kinachochukua nafasi ambapo watu hutafuta pato
kupitia njia zozote zile ikiwemo uhalfu.
Wakasema
kuwa kuna umuhimu wa uhalifu sababu unaileta jamii pamoja. Jamii inakuwa kwenye
kutafuta njia mwafaka kumaliza uhalifu, lakini lazima jamii hiyo ijitolesheleze
ndipo tunaweza kuufanya uhalifu kumalizika. .......
Naam
kama nchi yenu haiongelei suala la ukuzaji uchumi, itaongelea nini? Kama
tumeshuhudia watu kule Mwanza wanauana kisa HAKI YA KUCHINJA na kuvaa mavazi ya
DINI kisha kumwaga damu, nini tafsiri yako? Je, umewaona wanaoshiriki zoezi la
kuuana ni watu wa namna gani? ....je wale wanawezaje kuachwa katika faili la
UCHUMI? Hatuna uchumi imara lakini hatutakiwi kuacha kutafuta UCHUMI
imara.
@Nakupenda
sana nchi yangu TANZANIA.
Hatutendi
haki hata kidogo kutoandika 'aya' za uchumi wetu ambayo ndio msingi wa taifa
letu na kumwachia Rais wetu Kikwete akihutubia mambo machache. Labda afadhali
hayo machache kuliko kukosa kabisa. Kama tunataka kujenga utamaduni wa
kutomwambia basi tunajenga taifa la watu wasioweza kufikiri au taifa la watu
wanaopendelea mambo mepesi.
Hatukatai kuona kuwa hotuba ya rais wetu haiwezi
kuwaridhisha watu wote, lakini mimi naona kuna haja pia kuwakumbusha wale wote
wanaohusika kuwa, wajaribu na waweze kufanya kitu ambacho kinaakisi jamii yao.
Kama tunakubaliana kwamba uhalifu ni kitu kinacholeta jamii pamoja, na kwamba
lazima jamii ijitosheleze basi yatupasa kujiuliza itajitosheleza katika lipi na
kwanini?
Lazima tumfanye rais wetu awe 'mgumu' kwa maana mtu 'mzito' kwa hoja
nzito. Kwahiyo tusitegemee kuwa Rais anaweza kufanya hilo pekee bali lazima tusaidie,
lazima kumfanya awe bora sababu ni mali yetu na tunajivunia yeye. Lakini kama
kuna watu wanadhani kukosoa hotuba ya Rais ni dhambi ati sio saizi yetu hatuba
budi kusema labda akina sisi tunaokosoa tumechanganyikiwa na tunakaribia
kuchojoa nguo.
Ni jambo baya sana tunapoona kila mtu anadhani waandishi wa
hotuba ya Rais wanajua kila kitu. Lakini wanayo fursa ya kupata tafiti za
kisasa za uchumi, makabrasha na kadhalika ili kuweza kuelezea jambo la msingi
kuhusu hali ya maisha ya watu wetu.
Ni vigumu sana kuamini kuwa Rais wetu
anaandikiwa hotuba nusu, labda wenzetu walisahau, ila nakumbusha kama huijui
jamii yako basi unaelekea kuchanganyikiwa. Turuhusu waandishi wa hotuba ya rais
wawe hodari kwa kuwajengea hoja zenye maana sio kuwatusi. Tuwape nafasi ya
kujisahihisha sababu wao sio miungu hata kidogo..
No comments:
Post a Comment
Maoni yako