September 22, 2017

KITONGOJI FEKI CHAGUNDULIKA NDANI YA HIFADHI NYASA

NA ALBANO MIDELO, NYASA

NYUMBA 25 zilizokuwa na kaya 65 ambazo zilijengwa katika hifadhi ya msitu milima ya Ruhekei katika Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma zimebolewa na kuondolewa ndani ya hifadhi hiyo.

Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bugingo Bugingo amesema zoezi la kubomoa nyumba hizo katika hifadhi hiyo limedumu kwa miaka mitatu na kwamba zoezi limefanyika kwa amani na utulivu kwa njia ya kidiplomasia hadi wananchi hao walipoamua wenyewe kubomoa nyumba zao na kuondoka hifadhini mwezi Agosti 2017.


Hifadhi ya msitu wa Ruhekei yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 2000,ndiyo hifadhi kongwe kuliko zote katika katika mkoa wa Ruvuma ambayo ilianzishwa rasmi na kutangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1938.
Hifadhi hiyo ni muhimu kwa sababu ni chanzo muhimu cha maji ukiwemo mto Ruhekei ambao unamwaga maji yake ziwa Nyasa.Mto huo pia ni mazalia muhimu ya samaki aina ya ngisi na mbelele.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako