November 30, 2017

UGONJWA WA KIPINDU PINDU UMEINGIA WILAYA YA NYASA

NA MWANDISHI WETU, MBAMBA BAY
 
UGONJWA wa Kipindupindu umebisha hodi kwa mara nyingine kama ilivyokuwa mwaka jana wilayani Nyasa, ambapo watu mbalimbali walikimbizwa hospitali kutokana na kuharisha na kutapika.
Wauguzi katika Zahanati ya mbamba Bay

Taarifa zinasema kuwa katika maeneo mengi wilayani Nyasa kwa sasa kuna ugonjwa hatari wa kipindupindu hususani vijiji vya Mwambao wa Ziwa Nyasa  upande kusini mwa wilaya hiyo kuanzia Kwambe hadi Liuli.
Taarifa hizo zinabainsha kuwa Kijiji cha Kwambe watu watatu (3) wamefariki dunia hadi kufikia siku ya Jumanne wiki hii. Mbali na hivyo, watu Ishirini (20) wamelazwa katika Zahanati ya Chiulu hadi sasa. 

 AIdha, ugonjwa huo umeshika kasi pia katika Kijiji cha Lundo, kilichoko Kata ya Lipingo, pamoja na Chinula na maeneo mengineyo. Kata ya Lipingo inatajwa kuwa hali mbaya zaidi kwani hadi jnaa Jumanne jioni watu 6 wamefariki, hali ambayo imechochea kuongezwa wataalamu katika Zahanati ya Lundo, pamoja na vifaa vya tiba na magodoro ili kuongeza tija kwani kituo cha Afya cha Makwai kilichopo katika kijiji cha Lundo kimelemewa. Maeneo mengineyo nayo wagonjwa wamelazwa katika Hospitali ya Liuli. 

ANGALIZO:
Tuweke mazingira yetu safi, Tusile vyakula vya baridi (vimbala na michuzi ya maji na chumvi), tuache unywaji pombe Kiholela hususani za Kienyeji (komoni na wanzuki - Viporomba). Matumizi mazuri ya vyoo, kunawa kila utokapo chooni, kuosha maembe kabla ya kula, pia kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa.
MATIBABU : Ukiona dalili za kuhara mfululizo au kutapika Basi wahi mapema Kituo cha Afya kilichoko jirani nawe.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako