December 06, 2017

“KURUDI NYUMBANI”, IMERUDI STARINI TENA"

MWAKA 2012 nilianzisha kipengere cha “KURUDI NYUMBANI” katika blogu hii. Mtu wa kwanza kuhojiwa alikuwa Ambroce Nkwera. Unaweza kusoma mahojiano hayo kwa KUBONYEZA HAPA. 

Labda swali hapa ni kwanini nilianzisha kipengere cha “KURUDI NYUMBANI”?  Kwanza, Sababu kubwa ni kwamba kuna wafanyakazi waliowahi kuajiriwa na kupangiwa wilaya ya Mbinga ama maeneo ya Wilaya za mkoa Ruvuma halafu hawaendi kufanya kazi vituo vya kazi. 

Hilo lilikuwa tatizo kubwa hivyo niliazimia kuona kuna haja wazaliwa wa maeneo hayo wenye sifa kuomba kazi ili warejee na kuwatumikia watu wa nyumbani kwao. 

Pili, dhana hii ilikuwa kuzungumza na wazaliwa wa wilaya Nyasa wenye utaalamu wa aina mbalimbali kutoka darasani au elimu dunia. Kwa kipindi cha miaka minne sijawahi kukifanyia kazi kipengere hiki hivyo ninadhani ni jambo zuri zaidi kuiendelea kuzungumza na wasomi wa nyumbani Nyasa, mawazo yao na maoni yao juu ya kuboresha  maisha ya wilaya hiyo na kadhalika.
KUNA MAPYA …….VUTA SUBIRA……

Mhariri 
Markus Mpangala


No comments:

Post a Comment

Maoni yako