February 15, 2018

ABDUL-RAHMAN IBRAHIM BIN SORI: MTUMWA WA GUINEA ALIYEOKOLEWA NA SULTAN WA MOROCCO.

Na KIZITO MPANGALA

Abdu-Rahman Ibrahim bin Sori alizaliwa mwaka 1762 katika mji wa Timbo kitongoji cha Futa Djallon (sasa ni nchi ya Guinea) huko Afrika Magharibi katika jamii ya kabila la Fulani. Baba yake alikuwa mfalame wa mji wa Timbo (Guinea) na hivyo Abdul-Rahman alikuwa ni mwanamfalme (Prince)
Katika makuzi yake alipelekwa mjini Timbuktu kujifunza masuala yanayohusu dini ya Kiislamu. Akiwa mjini Timbuktu, Adul-Rahman alijifunza lugha nne za makabila ya Afrika Magharibi pamoja na lugha ya Kiarabu na aliporudi mjini timbo alijiunga na jeshi la baba yake ambaye alikuwa kiongozi wa kitongoji cha Futa Jallon mjini Timbo (sasa ni Guinea).

Abdul-Rahman alipofikisha miaka 26 alifanywa kuwa kiongozi wa jeshi hilo liliokuwa na askari 2000. Kazi yake kuu katika jeshi hilo ilikuwa kuhakikisha ulinzi wa pwani yote ya Timbo (Guinea) umeimarika na kuliweka jeshi lake tayari kwa kupambana na adui yeyote ambaye angeivamia pwani hiyo.
Kutokana na uwezo wake wa kijeshi, Abdul-Rahman aliwindwa sana na wazungu wa Uingereza ambapo mwaka 1788 wazungu hao walifanikiwa kumteka na kusafiri naye hadi katika mji wa Mississippi nchini Marekani kisha aliuzwa na kuwa mtumwa. Akiwa mjini Mississippi laitumikishwa kufanya kazi katika mashamba ya pamba ya tajiri Thomas Foster kwa zaidi ya miaka 38 kabla ya kuachiwa huru.

Kutokana na uwezo wake katika kilimo cha pamba alichokuwa akifanya huko Mississippi, Abdulrahman alikuwa akijishughulisha pia na kilimo cha bustani ya mboga za majani, bustani hiyo ilikuwa ni ya kwake mwenyewe. Na mwaka 1894 alimuoa binti Isabella mtumwa mwenzake katika mashamba ya pambo walimokuwa wakifanya kazi.

Abdul-Rahman alibahatika kupatana vizuri na dakitari wa merikebu ya Waingereza, John Cox ambaye alimkaribisha nyumbani kwake mara kwa mara kwa kuwa kwa mara ya kwanza walionana katika pwani ya mji wa Timbo (Guinea) wakati alipotekwa na Waingereza hao. Dokta John Cox alimuomba tajiri wa mashamba ya pamba, Thomas Foster kumuachia huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori ili arudishwe kwao Timbo (Guinea) lakini tajiri huyo alikataa kufanya hivyo kwa kuwa Abdulrahman alikuwa mchapakazi hodari katika mashamba hayo. Dokta John Cox aliendelea kubembeleza kwamba Abdul-Rahman aachiliwe huru mpaka alipofariki bila mafanikio ya ombi lake. Baada ya dokta John Cox kufariki, kijana wake wa kiume alikendeleza kubembeleza kwamba Abdurahman aachiliwe huru.
Mwaka 1826 Abdu-Rahman Ibrahim bin Sori aliandika barua kwa ndugu zake huko Timbo (Guinea). Baada ya kuiandika barua hiyo, ilichukuliwa na Andrea Marschalk ambaye alikuwa Mdachi na kazi yake ilikuwa ni katibu muhtasi. Barua hiyo ilipelekwa kwa Seneta wa jimbo la Mississippi, Thomas Reed ambaye alikuwa katika matembezi yake wakati huo kuelekea mjini Washington, hivyo aliibeba barua hiyo na kuipeleka kwa Balozi wa Marekani nchini Morocco na kisha kupelekwa mjini Timbo (Guinea). Ilipelekwa nchini Morocco kwa sababu Abdul-Rahman aliiandikwa kwa lugha ya kiarabu, hivyo alidhaniwa kuwa ni mwenyeji wa Morocco.
Barua ilipokelewa na kupelekwa kwa Sultan wa Morocco. Baada ya Sultan kuisoma barua hiyo, alituma ombi la kuachuliwa huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori. Ombi hilo lilitumwa kwa Rais wa Marekani wakati huo, John Quincy Adams.
Mwaka 1829 tajiri wa mashamba ya pamba, Thomas Foster alikubali kumuachiliwa huru Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori bila kumpa ujira kwa kazi aliyoifanya mashambani humo, kwa makubaliano kwamba arudi Afrika na siyo kubaki Marekani akiwa huru.
Abdul-Rahman na mkewe kabla hawajaondoka Marekani, walizunguka katika miji mingi ukiwemo Washington D.C ambapo alionana ana kwa ana na Rais John Quincy Adams. Abdul-Rahman aliomba kubaki kwa muda mjini Mississippi ili ajiandae na familia yake kurudi Afrika. Taarifa hii ilimfikia tajiri Thomas Foster ambaye alichukulia taarifa hii kuwa Abdu-Rahman amekiuka mkataba aliokubaliana naye.
Miezi kumi baadae, Abdul-Rahman na mkewe Isabella walikuwa wamepata nusu ya fedha kwa ajili ya kulipia uhuru wa watoto wao ili wasiwe watumwa Mississipi nchini Marekani wakati wao wakirudi Afrika. Baada ya kufanya hivyo, Abdul-Rahman na mkewe Isabella walirudi Afrika na kufikia mjini Monrovia, Liberia bila watoto wao. Abdul-Rahman Ibrahim aliishi kwa muda wa miezi miine tu nchini Liberia na kufariki kutokana na kuugua kwa muda mrefu. Hakuiona tena Timbo, Futa Djallon wala watoto wake tena.
Fedha ambazo walizipata walipokuwa Mississippi walilipia uhuru wa watoto wao wawili tu ambao baadaye waliwasili mjini Monrovia, Liberia na kuishi na mama yao, Isabella. Naye tajiri wa mashamba ya pamba mjini Mississippi, Thomas Foster alifariki mwaka huo huo ambao alifariki Abdul-Rahman Ibrahin bin Sori na ukwasi wake uligawanywa kwa mtoto wake na watoto na wajukuu wa Abdul-Rahman ambao alibaki katika kasri ya tajiri huyo kama watumw. Baada ya kugawana, walisambaa maeneo mbalimbali kusini mwa Mississippi.
Mwaka 1977, Profesa wa Historia, Terry Alford aliandika kitabu kilichokuwa na simulizi ya maisha ya Abdul-Rahman tangu alipokuwa Afrika hadi alipotekwa na kurudi tena Afrika. Kitabu hicho kinaitwa PRINCE AMONG SLAVES.
Mwaka 2006, kizazi cha Abul-Rahman na kizazi cha Thomas Foster viliungana kama wanafamilia katika kasri ya Thomas Foster na kuishi pamaoja katika kasri hiyo na kushika maeneo yote ya mashamba ya pamba.
Mwaka 2007, mwongozaji wa filamu nchini Marekani, Andrea Kalin alitengeneza filamu iliyokuwa ikisimulia maisha ya Abdul-Rahman Ibrahim bin Sori na kutolewa rasmi mwaka 2008. Filamu hiyo imebeba jina la kitabu kilichoandikwa na Profesa Terry Alford, PRINCE AMONG SLAVES.
0692 555 874  

No comments:

Post a Comment

Maoni yako